Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NUSU ya idadi ya raia wa China ambao wamefikia zaidi wa watu milioni 780 wamekumbana zuio la kusafiri ikiwa ni sehemu ya mlengo wa Mamlaka husika inayoendelea  kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona (Covid 19)

Tangu virusi hivyo vimeikumba nchi hiyo takribani watu 1,770 wamepoteza maisha huku watu 70,000 wakiwa wameambukizwa virusi hivyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la Utangazaji CNN imeelezwa kuwa kumekuwa na zuio la safari na msisitizo kwa watu kubaki katika miji  yao.

Zuio hilo imehusisha kila kitu kutoka kwa kila anayekuja na kuondoka kutoka maeneo jirani.

Baadhi ya marufuku iyo imeonekana katikka miji minne katika eneo la  Hubei ambako vifo 100 zaidi viliripotiwa siku ya jumapili.

Katika miji ya Wuhan, Huanggang, Shiyan na Xiaogan kumewekwa mazuio  katika maeneo yote yaliyosalia wakazi huku matumizi ya magari katika barabara yamepigwa marufuku huku makazi katika miji yamekuwa yakipokea mahitaji kutoka kwa majirani na kamisheni  za kijamii baada ya kuzuiwa kutoka majumbani mwao.

Jumapili Hubei ilitangaza hatua mpya za vizuizi vya maeneo yote kwa safari  zote zisizo za dharura pamoja na magari yasiyo na dharura  kupita katika mitaa ya umma na tayari imeripotiwa kwa baadhi ya maeneo hakuna aliyeruhusiwa kutoka nje ila kwa dharura maalumu.

Pia wataalamu wamekuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuangaalia afya pamoja na kuhakikisha kama kuna kisa kipya huku mamlaka zikisisitiza kuwa kwa yeyote atakayebainika kuwa na dalili za awali aripotiwe kwa Serikali za vijiji na jamii ili apate huduma kwa urahisi na haraka katika vizuizi vyao na sio kubaki nyumbani.

Kwa upande wa uchumi, Hubei imesema kuwa kampuni hazifai kuanza tena uzalishaji isipokuwa kwa ruhusa ya mamlaka ya kuzuia janga hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...