Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dk. Sophia Mjema (katikati) akionesha cheti cha shahada ya heshima ya udaktari alichotunukiwa na Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' (LeadImpact University) cha nchini Marekani kwa kutambua mchango wake katika kuihudumia jamii kwenye majukumu yake. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Dk. Christina Onyango ambaye pia katunukiwa udaktari wa heshima na chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dk. Sophia Mjema akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' (LeadImpact University) cha nchini Marekani kwa kutambua mchango wake katika kuihudumija jamii kwenye majukumu yake.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' cha nchini Marekani, Askofu Mkuu Cletus Bassey akizungumza katika hafla ya kuwatunuku shahada ya udaktari wa heshima jijini Dar es Salaam.
Askofu Richard Harper toka Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' cha nchini Marekani akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa wahitimu ambaye ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Dk. Christina Onyango akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutunukiwa udaktari wa heshima na chuo cha LeadImpact University cha nchini Marekani.
Mmoja wa watunukiwa wa shahada ya udaktari wa heshima toka LeadImpact University, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Dk. Jumaa Mhina akizungumza kukishukuru chuo hicho kwa kutambua mchango wa Watanzania hao kwa jamii.
Wanamahafali wa Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' (LeadImpact University) wakiandamana kuingia katika Ukumbi wa Karimjee kutunukiwa...!
Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiwaongoza Wanamahafali wa Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' (LeadImpact University) kabla ya kutunukiwa...!
Sehemu ya wageni waalikwa katika mahafali hayo...
Mkuu wa Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' cha nchini Marekani, Askofu Mkuu Cletus Bassey (kushoto) akimtunuku Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Dk. Christina Onyango udaktari wa heshima.

Sehemu ya wanamahafali wa Chuo Kikuu cha 'LeadImpact' cha nchini Marekani wakiwa katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...