Kampuni Life Line Engeneers  imetoa Mafunzo kwa wanawake wa uhandisi umeme 11 kufanya matengenezo ya umeme bila kuzima.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Donald Mwakamele amesema Mafunzo hayo ni endelevu kwa wanawake ili waweze kuwa mahiri katika kazi ya uhandisi umeme .

Amesema kuwa kuzima umeme wakati wa kufanya matengenezo ni hatari hivyo Mafunzo yanayotolewa yatasaidia kuongeza ujuzi.

Mwakamele amesema kuwa katika uchumi wa Viwanda haiwezekani ukazima kiwanda kwa sababu ya kufanya matengenezo.

"Uchumi wa Viwanda unahitaji kuwa na nguvu kazi yenye maarifa ya kutatua tatizo bila kusimamisha uzalishaji unaotokana na umeme"amesema Mwakamele.

Amesema kuwa utaratibu uliotumika ni wanawake kuomba  ambao wamefanyiwa  ni wale ambao waliomba.

Mwakamele amesema kwanza wamefanya  matengenezo ya umeme ikiwa ni pamoja na kubadilisha nguzo bila kuzima umeme wenye msongo wa 11kilovots katika eneo la hospital ya Agakhani Jijini Dar es saalam.
Wanawake wakifanya matengenezo ya umeme  bila kuzima. 
Baadhi ya wanawake wakiwa wameketi mara baada ya kushiriki Mafunzo ya Kutengeneza uunganishaji wa umeme bila kuzima 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...