Timu ya madaktari 35 wa Kichina wanaendelea na kampeni yao ya kutoa mafunzo mjini Khartoum, Sudan, juu ya jinsi ya kuepuka maambukizi ya virusi hatari vya corona na njia za kutibu ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.

Maafisa zaidi ya 50 wa afya nchini Sudan wanashiriki katika zoezi hilo ambalo lengo lake kuu ni kuchukua hatua za haraka za kuzuia na kutibu ugonjwa huo hatari.

Mmoja wa madaktari hao kutoka China, Li Changhong, amesema kuwa, timu yake ina mawasiliano ya karibu na Wizara ya Afya ya Sudan kuhusu ugonjwa huo na imetumwa mjini Khartoum kutoa mafunzo kwa hospitali za mji huo juu ya hatua za kuchukuliwa za kuzuia, kudhibiti na kupiga karantini. #CORONAVIRUS
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...