Yassir Simba,  Michuzi tv

Namungo waendelea kuutumia vyema uwanja wao nyumbani wa Majaliwa Stadium wilayani Ruangwa mkoani Lindi mara baada ya leo tarehe 22 mwezi wa February mwaka 2020  kuwaadhibu wana lambalamba Azam Football club.

Mchezo huo uliyokuwa na kasi kubwa na kosakosa ya mashambulizi kwa timu zote ambapo dakika 45 za kipindi cha kwanza tulishuhudia timu zote mbili zikitoka suluhu ya bila kufangana

Ambapo iliwachukua dakika 60  za mchezo wakulima wa korosho kupitia kwa Reliants Lusajo ilitosha kuwaadhibu wanalambalamba Azam Football Club.

Mpaka dakika 90 za michezo Namungo 1 Azam Football club 0 baada ya mchezo huo rasmi Namungo wanajikita nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 23 wakivuna alama 43 huku Azam akibaki nafasi ya pili akiwa na alama 45 baada ya michezo 24 huku nafasi ya kwanza ikiendelea kumilikiwa na Simba Sports Club wakiwa na alama 59 mara baada ya michezo 23.

Rasmi Mshambuliaji wa Namungo Fc Reliants Lusajo anafikisha magoli 10 akizidiwa magoli 2 na Kinara wa mabao Meddy Kagere mwenye magoli 12.
 Kikosi cha Namungo FC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...