Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa
Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya
Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya
kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia
mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya
udalali kwa mujibu wa Sheria.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akizindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji
Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara
(GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo
madalali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo kuwasilisha maombi
yao ya leseni.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa
Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya
Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya
kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia
mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya
udalali kwa mujibu wa Sheria.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akizindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji
Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara
(GAMIS Portal-Auctioneers License), ambapo madadali wote wanatakiwa
kuanza kuutumia kuwasilisha maombi ya leseni zao kupitia mfumo huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akimkabidhi leseni ya udalali iliyotolewa kwa
njia ya Kieletroniki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono
Bi. Scholastika Kevela, mara baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo wa
Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya
Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es
salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akizungumza na wawakilishi wa madalali pamoja
na wahakiki mali wa mikoa Tanzania Bara kabla ya kuzindua Mfumo wa
Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya
Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es
Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo
kuwasilisha maombi yao ya leseni.

Mwenyekiti wa Madalali wa
Mahakama Tanzania Bara Bi. Mwamvua Kigulu (kushoto) akizungumza jambo
kwa niaba ya madalali wa mahakama wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa
Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya
Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es
Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo
kuwasilisha maombi yao ya leseni.

Mwenyekiti wa Madalali Binafsi
Tanzania Bara Bw. Phidel Katundu (kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya
madalali binafsi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji
Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara
(GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini dar es Salaam, ambapo
madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo kuwasilisha maombi
yao ya leseni.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi mbalimbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya
Madalali na Wahakiki mali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara mara baada
ya kuzindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na
Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers
License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza
kuutumia mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………………………………………………………
Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar Salaam
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James mewaonya madadali na
waendesha minada Tanzania Bara kuacha mara moja kufanya biashara hiyo
bilaa kujisajili kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Bw. James
ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizundua Mfumo Mpya wa
Kieletroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ya
hadhara Tanzania Bara ambapo watoa huduma hiyo kuanza sasa wanatakiwa
kujisajili kupitia mfumo huo kwa njia ya mtandao wa Internet ama kupitia
simu zao za kiganjani.
‘’Napenda
kuwafikishia taarifa hii wananchi wote, hasa Madalali na waendesha
minada, kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kufuatilia na
kuchukua hatua kali kwa wote watakaojuhusisha na shughuli za udalali na
uendeshaji wa minada bila kuwa na leseni halali’’ alisema Bw. James.
Aliziagiza
Taasisi zote za Serikali kufanya kazi na Madalali na waendesha minada
ambao wanatambulika kisheria na kwa kufanya hivyo watakuwa wameisaidia
Serikali kujipatia mapato yatakayotokana na ada ya leseni itakayolipwa
na wafanyabiashara ya udali na waendesha minada.
“Mfumo huu
utapunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zinatumia
mlolongo mrefu wa kupata leseni kwa kuwa mfumo huo umeunganishwa na
Mfumo wa Malipo wa GePG ambapo mwombaji ataweza kulipia ada ya leseni
kwa kutumia benki, mawakala au simu za kiganjani na hivyo kurahisisha na
kuboresha ulipaji, kupunguza gharama za ulipaji na kuongeza uwazi na
udhibiti wa Fedha za Umma.
Bw. James
aliutangazia Umma kuwa kuanzia tarehe 24 Februari, 2020 maombi yote ya
leseni za Udalali na Uendeshaji wa Minada Tanzania Bara yawasilishwe
kupitia Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada ambao
unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango (www.mof.go.tz);
Awali, Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo,
amesema biashara ya udalali na uendeshaji wa minada hapa nchini imekuwa
ikikua kwa kasi na hivyo kutengeneza ajira, kuongeza kipato pamoja na
kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Bw. Chotto
aliongeza kuwa leseni za Udalali na uendeshaji wa minada Tanzania Bara
zinatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mujibu wa sheria ya
waendesha minada ya Mwaka 1928 iliyorejewa Mwaka 2002, na Wizara imekuwa
ikifanya jitihada mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wadau
hawa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Wakizungumza
kwa niaba ya madalali, Mwenyekiti wa Chama cha Mdalali wa Mahakama Bi.
Mwamvua Kigulu na Mwenyekiti wa madalali Binafsi Bw. Phidel Katundu,
wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kubuni
mfumo huo utakao wapunguzia gharama ya kufuata huduma ya usajili jijini
Dodoma.
Wameiomba
Serikali kudhibiti madalali wasio na leseni au wale wasiosajiliwa kwa
kuwa wanaikosesha Serikali mapato pamoja na kuchafua taswira ya biashara
ya udalali nchini.
Wamemwomba
Katibu Mkuu Bw. Doto James kupitia upya Sheria ya Udalali ya Mwaka 1928
ambayo wamesema imepitwa na wakati na inakwaza shughuli za udalali
nchini ikiwemo urasimu wa ufanyakazi kazi zao kutoka kwa mamlaka za
Serikali Kuu hasa makatibu Tawala wa Wilaya ambao wanataka kupata vibali
kutoka kwao kabla ya kutekeleza kazi zao za udalali katika maeneo
husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...