Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara nyingine tena imeshindwa kusoma hukumu ya kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo na mwenzake Micke William kwa sababu Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo leo amepata udhuru.

Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilipangwa kutolewa hukumu Novemba 26, mwaka 2019 lakini iliahirishwa kutokana na Hakimu kutomaliza kuandaa hukumu na kupanga Desemba 29 hata hivyo iliahirishwa kwa sababu hiyo hiyo.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa tena Januari 22, mwaka 2020 lakini haikuweza kutolewa na kuahirishwa hadi Februari 19.Hata hivyo Hakimu anaesikiliza kesi hiyo Thomasi Simba leo hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai leo Februari 19,mwaka 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi ,kuwa kesi hiyo ilipangwa kwaajili ya kutolewa hukumu lakini Hakimu husika hayupo kutokana na majukumu mengine. Wakili wa utetezi Peter Kibatala alidai wako tayari kwa hukumu lakini kutokana na maelezo ya Wakili wa Serikali hawana pingamizi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 19 mwaka 2020 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na hukumu itasomwa Aprili 2, mwaka huu. Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, kinyume na Sheria namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...