Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kushiriki katika Swala ya Ijumaa kwenye Msikiti
wa Gaddafi mjini Dodoma, Februari 14, 2020. Katikati ni Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na wazee baada ya kushiriki katika Sala ya Ijumaa kwenye
Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma, Februari 14, 2020. Wa pili kulia ni
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na kulia ni Sheikh wa
Mkoa wa Dodoma, Alhaj Mustafa Rajab Shaaban.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi wakisalimiana na Sheikh
wa Mkoa wa Dodoma, Alhaj Mustafa Rajab Shaaban (katikati) baada ya
kushiriki katika Swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Gaddafi jijini
Dodoma, Februari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi baada
ya kushiriki katika Swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Gaddafi jijini
Dodoma, Februari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amewaasa wanasiasa nchini kutotumia mlipuko wa virusi
vya corona uliotokea China na kuua watu zaidi ya 1,400 kujipatia
umaarufu wa kisiasa.
Hivyo, Waziri
Mkuu amewataka Watanzania waendelee kuitegemea Serikali katika kupata
taarifa za mara kwa mara kuhusu masuala mbalimbali zikiwemo na za
mlipuko wa virusi hivyo. “Tusiupoteshe umma.”
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 14, 2020) mara baada ya kushiriki
swala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma. Amesisitiza
umuhimu wa wananchi kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aliepushe na
maafa mbalimbali.
Waziri Mkuu
amesema kazi inayofanywa na Serikali kwa sasa nchini ni kuhakikisha nchi
inaendelea kuwa salama, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi
waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aliepushe Taifa na maafa mbalimbali
ikiwemo mlipuko wa corona, baa la nzige na mafuriko.
Amesema
katika mji wa Wuhan ambako virusi hivyo vilianzia, wapo vijana 497 wa
Kitanzania huko na wote wapo salama na Serikali inaendelea kuwasiliana
nao kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi za ubalozi.
“Taifa hili
ni muhimu sana kwetu na ni msingi wa maisha yetu, hivyo watu wasiwe
wanapotosha umma na kuwatia hofu Watanzania, vijana wetu wapo salama.
Pia tumejipanga kukabiliana na majanga hayo ikiwa ni pamoja na nzige.
Tumuombe sana Mwenyezi Mungu atuepushe”
Kadhalika,Waziri
Mkuu ametoa wito kwa wananchi wawasikilize viongozi wa dini na
waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu awape uvumilivu na waliombee Taifa
lidumishe amani.
“Viongozi wa
dini muendelee kuhamasisha uwepo wa amani nchini. Taifa linaendelea kuwa
na amani kutokana na mawaidha yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa
dini.”
Waziri Mkuu
ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wanzania waendelee kushikamana na
wafuate maelekezo yanayotolewa na viongozi wa dini ili waweze kujenga
msingi imara kwa vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...