Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amefanya kikao na wakurugenzi na viongozi wa taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya viwanda na biashara.
Kikao hicho wameshirikisha viongozi mbalimbali wa wizara ambao ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stella Manyanya, Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki S. Shemdoe na viongozi mbalimbali wa wizara ya viwanda na biashara na taasisi zake.
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadili utekelezaji wa Vipaumbele na mikakati ya kazi kwa kila taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2020/2021.



Pichani kati ni Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho cha Wakurugenzi na viongozi wa taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya viwanda na biashara.Pichani kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Stella Manyanya na kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki S. Shemdoe
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Stella Manyanya akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kikao hicho


Kikao kikiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...