Mkufunzi Mkuu wa KAIZEN (AKT) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Jane Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa mafunzo ya mfumo wa KAIZEN jijini Dar es Salaam leo.

MASHINDANO ya nne ya KAIZEN kufanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Wizara ya Viwanda na biashara, Innocent Bashungwa.

Mashindano ya KAIZEN kwa hapa nchini yamekuwa yakifanyika kila mwaka ifikapo Februali, 18, kwa mwaka huu yanalengo la kubadilishana uzoefu na kuhamasisha ushiriki wa wadau kwenye uenezaji wa falsafa ya KAIZEN kwa nchi nzima.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo ya KAIZEN jijini Dar es Salaam leo kwa waandishi wa habari, Mkufunzi Mkuu wa KAIZEN (AKT) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Jane Lyatuu amesema mwaka huu utekelezaji wa mradi wa KAIZEN ni kwa mikoa nane (8).

Jane ameitambulisha mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Morogoro, Singida, Mbeya na Mwanza.

"Mashindano haya yatafatiwa na sherehe za kukabidhi tuzo kwa washindi zitakazo anza saa nane mchana, kupata nshindi atakayewakilisha Tanzania katika Barani Afrika, yatakayofanyika nchini Afrika Kusini."Amesema Jane

Mashindano ya KAIZEN hapa nchini viwanda 14 vimechaguliwa kushiriki mashindano hayo kwa mwaka huu na washiriki ni zaidi ya 150, wakiwemo wazalishaji wa viwandani, washauri elekezi,viongozi na maafisa serikali na wakufunzi wa KAIZEN, wanahabari, wawakilishi kutoka shirikisho la viwanda Tanzania (CTI), Sekta binafsi nchini, Jumuia ya watu wenye viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA) na Jumuia ya wanawake wafanyabiashara nchini (TWCC).

Kwa wananchi wasiojua maana ya KAIZEN, KAIZEN ni falsafa kutumia mbinu bunifu ya uimarishaji endelevu wa tija ya ubora viwandani ambayo inazingatia usimamizi na matumizi bora ya rasilimaliwatu, fedha, muda na miundombinu ili kupunguza upotevu wa gharama zisizokuwa na lazima viwandani na hatimaye viwanda kuweza kuhimili ushindani wa biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...