Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Makao
Makuu ya Wizara na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (hawapo pichani)
katika Kikao cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo,
kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (wapili kulia) akimuuliza swali Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule (kushoto),
katika Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Makao Makuu ya Wizara na
NIDA cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo,
kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Wapili kushoto ni
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Makao
Makuu ya Wizara na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Kikao cha
kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo, kilichofanyika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza na Wakuu wa Idara na
Vitengo wa Makao Makuu ya Wizara na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) katika Kikao cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya
Maendeleo, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma,
leo. Kushoto meza kuu ni Waziri wa Wizara hiyo, George Simbachawene.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (wapili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Sera na
Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo (wapili kushoto), alipokuwa
anasoma taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Makao Makuu ya
Wizara katika Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa wa Wizara hiyo na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) cha kupitia Utekelezaji wa
Bajeti na Miradi ya Maendeleo, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Christopher Kadio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Arnold
Kihaule. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...