Muonekano wa hospitali ya Rufaa ya Temeke.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akitembelea maeneo ya ospitali ya Rufaa ya Temeke.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisikiliza wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, alipotemelea hospitali hiyo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
HOSPITALI ya Rufaa ya mkoa wa Temeke mbioni kufungwa mashine nne za Utra Sound  kwaajili kuongeza ubora wa huduma za Afya katika hospitali hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar ea Salaam leo.

Waziri Ummy alipofika katika Hospitali ya Temeke aliongea na wagonjwa waliokuwepo hospitali hapo.

Mmoja ya wangonjwa ametoa lalamiko hukusu ukosefu wa mashine za Utra Sound pamoja na mfumo wa malipo ambao haujakaa sawa.

Amepotolea majibu malalamko yao juu ya mashine hizo amesema kuwa mashine hizo zitafungwa katika hospitali hiyo.

Hata hivyo ametoa rai kwa wakazi wa jiji la Dar es Saalam kufuata  mfumo wa Rufaa na kutokukimbilia moja kwa moja katika hospitali ya Temeke.

"Nitoe rai kwa wakazi wa Dar es Salaam tufuate mfumo wa rufaa tusikimbilie moja kwa moja Temeke kuna baadhi ya huduma zinaweza zikapatikana katika vituo vya afya pamoja na hospitali ya wilaya. Sisi kama serikali tunaboresha vituo vya afya na katika vituo vyote vya afya, tutaweka mashine za  Utra Sound na kunabaadhi tumeshaanza kuweka mashine za RMO kwahiyo kwa kiasi kikubwa huduma za afya zote zitakuwa zinapatika katika vituo vya afya na Temeke ukija hapa tunataka kwaajili ya huduma za kibingwa." Amesema Waziri Ummy.

Na alipotembelea wagonjwa waliokuwa katika foleni ya dirisha la bima za afya hapo aliwashauri wananchi kutumia bima za afya ili kuepukana na gharama zisizo za lazima.

Hata hivyo waziri Ummy ameridhishwa na utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Temeke ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo kulikuwa na mapungufu.

"Mimi napenda kumpongeza Dkt. Shimwela tulimleta hapa septemba 2019 Temeke ya 2019 na ya 2020 ni tofauti amejiongeza kwa kupaka rangi majengo pamoja na kuanzisha huduma mbalimbali za kibingwa." Amesema Waziri Ummy.

Hata Waziri Ummy ametembelea wodi la wazazi na kuwapongeza madaktari na watoa huduma kwa kupunguza vifo vya kinamama.

"Kubwa ambalo tumeliona ni kupungua kwa vifo vya kinamama wajawazito 2018 vifo vya kinamama 16, 2019 vifo 8 lakini pia ukiangalia takwimu zao kuanzia Novemba 2019 hadi sasa hakuna mwanamke yeyote mjamzito ambaye amekuja Temeke akapoteza maisha, kwa hiyo hili sasa ninataka kuwapongeza Madaktari, wauguzi na watoa  huduma za Afya pamoja na maafisa Afya." Amesema Waziri Ummy.

Haya hivyo hospitali ya Rufaa ya Temeke kwa sasa inatoa huduma ya Afya ya meno.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dkt. Shimwela ameshukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwani minong'ono ya uzushi iliyokuwa ikiendelea kuhusiana na kubadilishana watoto hicho kitu hakipo kwa sababu ya uboreshaji wa huduma pamoja na vifaa mhimu vya kisasa vilivyoletwa.

"Hakuna mtoto ambaye alibadilishana kwa kuwa vipimo vya DNA na vifaa vya kisasa vinaonyesha."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...