Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema mchango wa sekta ya madini umezidi kuimarika hapa nchini na kwamba Serikali kwa upande wake imeridhishwa na utendaji kazi wa sekta hiyo kupitia Wizara ya Madini.

Ameyasema hayo leo Februari 23,2020 wakati akizungumza na wawekezaji katika sekta ya madini hapa nchini mkutano uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere(JNICC), jinini Dar es Salaam leo.

Amefafanua kuwa sekta ya madini hapa nchini imeendelea kuimarika na hivyo Serikali  inaridhishwa na utendaji wa sekta hiyo ya madini kupitia wizara yetu ya Madini pamoja na tume yetu ya madini Tanzania huku akifafanua kupitia taarifa ya pato la Taifa ya nusu ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 mchango wa sekta ya madini ulikuwa na kufikia asilimia 13.7 ambapo sekta hiyo imekuwa ya pili katika kuchangia pato la taifa.

"Katika kipindi cha nusu ya mwaka wa fedha serikali kupitia sekta ya madini imeweka kukushanya zaidi ya shilingi  bilioni 242 Sawa na asilimia 51.4 na kukusanya shilingi bilioni 470.89 ambayo ilitokana na vyanzo mbalimbali."

Amesema kuwa vyanzo vya kuingiza mapato ni mrahaba, ada ya ukaguzi wa madini, huduma za kimaabara, maizo ya machapisho ya kijiolojia pamoja na ada za leseni.

"Katika kukabiliana na utoroshwaji wa madini Serikali iliamua kuanzisha masoko ya madini kwa lengo la kuondoa mianya ya kufanya biashara ya madini kupitia nyia zisizo kuwa rasmi,"amesema  Waziri Mkuu Majaliwa Majaliwa

Ameongeza kuwa sasa kuna jumla ya masoko ya madini kwenye mikoa 27 na vituo vidogo vya ununuzi wa madini 28 kote nchini.Hata hivyo masoko hayo yamekuwa chachu katika kuimarisha na upatikanaji wa takwimu za madini ukilinganisha na hapo awali na masoko hayo yapo wazi kwa sote na kwa nchi za jumuiya ya maziwa makuu na kwa nchinzote za bara la Afrika na Duniani kwa ujumla kuja kuuza madini hapa Tanzania.

"Na masoko haya yanafanya kazi kwamsingi ya ushindani uwazi wa biashara pia niwahakikishie kuwa masoko yetu yana ulinzi na usalama wa kutosha na sifa zote zinazohitajika katika kufanya biashara hii ya madini hivyo basi endeleeni kutumia masoko hayo. Na hata kwa nchi ambazo hazi masoko endeleeni mkijipanga kuanzisha masoko kama mpango huo upo." Amesema Majaliwa.

Hata hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamehamasisha wamiliki wa migodi kuchangia zaidi katika huduma za jamii na kuimarisha shughuli zinazofanywa na wachimbaji wakibwa, wachimbaji wa kati na wachimbaji wadogo wa madini..

Pia serikali imeonesha ushiriki wa moja kwa moja katika kumiliki na kusimamia migodi na kumirikishwa kwa migodi kwa asilimia 16 ya hisa katika migodi pamoja na kuunganisha sekta ya madini pamoja na sekta nyingine za kiuchumi hapa nchini.

Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa sekretarieti zote za nchi mwanachama zinatekeleza makubaliano waliyojiwekea

Pamoja na kutoa taarifa za utekelezaji waka kama ilivyoidhinishwa kama walivyokubaliana.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020 alipowasili kufunga Mkutano huo wa Siku mbili uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere(JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Februari 23, 2020, ambapo Tanzania imezindua Cheti cha uhalisi cha madini ya bati. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...