WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amezindua cheti cha Uhalisi wa madini ya Bati ambapo amesema uzinduzi huo ni muhimu kwa Taifa letu pamoja na nchi za maziwa makuu.

Amezidua cheti hicho cha uhalisi wakati wa mkutano wa wawekezaji katika sekta ya madini hapa nchini mkutano uliofanyika leo Februari 23,mwaka 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar ea Salaam.

Nchi mbalimbali zimepata Cheti cha halisi wa madini ya Bati ambazo ni Uganda, Burundi, Kenya, Zambia, nchi ya Afrika ya Kati, Sudani, Angola, Congo, Rwanda pamoja na Jamhuri ya Sudani.

Hata TANZA Plus wamepata zawaidi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera akipata cheti cha uhalisi wa madini bati pamoja na zawadi kwa kuwa Wilaya ya Kerwa Mkoani Kagera ndipo madini hayo yanapochimbwa.

"Napongeza uzinduzi wa cheti cha uhalisia wa madini bati, (origin certificate) ambayo yanapatikana wilaya ya Kerwa mkoani Kagera na maeneo mengine yanayozalisha bati," amesema Majaliwa na kuongeza cheti hicho kitaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kupata cheti hicho cha Uhalisia wa madini bati.

Hata hivyo Majaliwa amesema kuwa uzinduzi wa cheti hicho ni mhimu kwa taifa letu na nchi wanachama  wa maziwa makuu kwa sababu itaanza kudhibiti na kufata taratibu za kufata madini hayo, uwekezaji pamoja na kupata masoko yake.

Pia Waziri Mkuu  Majaliwa ametoa rai kwa nchi wanachama kuandaa mkutano wa kuwakutanisha wawezezaji wa nchi mwanachama wa maziwa makuuna kutoa fursa zilizopo  katika sekta ya madini.

 Ametumia nafasi hiyo kuitaka Wiizara ya Madini kuandaa mikutano mingine mingi ili kupanua uelewa wa pamoja wa wadau wa madini ili kuongeza pato la Taifa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha cheti baada ya kuzindua  utoaji wa  cheti cha uhalisia   kwa Madini ya Bati kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 23, 2020. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai, wa pili kushoto ni Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto ni  Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Maendeleo ya Madini wa Uganda,  Sarah Opendi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akikata utepe kuzindua  Utoaji wa Cheti cha Uhalisia kwa Madini ya Bati kwenye  ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 23, 2020.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...