Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMATI ya Bongomovie imempa siku tano Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa kuwaomba radhi wasanii kufatia maneno aliyozungumza Bungeni mnamo Febuari 3 mwaka huu wakati akichangia hoja katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steven Mengere al maarufu kama Steve Nyerere amesema Mbunge huyo ameshindwa kutambua mchango wa Wasanii katika kuleta maendeleo pamoja na kutangaza Utalii nchini Tanzania.
"Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla alituamini na akatupa kazi ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini na mwaka jana tulifanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro japo wengi wetu hatukufika kileleni kabisa lakini kwa namna moja au nyingine kupitia sisi wasanii tumeamsha hari kwa wenyeji na wageni kuhamasisha na kuona ipo fursa ya kufanya utalii katika nchi yetu", amesema Steve.
Hata hivyo Steve ameeleza kuwa ifike wakati viongozi na mashirika binafsi waheshimu kazi za sanaa kwani ni mojawapo ya kuleta ushawishi kwa watu kupitia kazi zao.
"Inapofanyika mikutano hasa kampeni, Wasanii wamekuwa wakitumika ili kuleta hamasa kwa wananchi hata yeye tulifika jimboni kwake nakufanya kampeni ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo," ameeleza Steve.
Kwa upande wake Katibu wa Uzalendo Kwanza, Kulwa Kikumba a.k.a Dude amesema Kamati hiyo imekaa na kushauriana na kumpa siku tano Mbunge huyo kuomba radhi kwa kile kinachodaiwa kuwa amemdhihaki Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere kuona hana mchango katika kutangaza utalii.
"Sanaa ni mojawapo ya Sekta ambayo inazalisha watu wakubwa na watu hao wengi wetu tunaendesha maisha yetu na familia zetu kupitia kazi za sanaa tunaomba iheshimiwe ichukuliwe kama kazi zingine", Dude
Pia Dude ameeleza kuwa alikuwa Msanii wa kwanza wa Bongomovie kufika kilele cha mlima Kilimanjaro na amepata fursa kwa namna moja au nyingine kuutangaza utalii kupitia nafasi hiyo aliyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Kigwangwala.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...