WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amevuliwa uanachama pamoja na madaraka na  kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini 

Hayo ameyasema, Katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole leo Februari 28, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi (CCM),Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati Membe akivuliwa uanachama, katibu mkuu wa zamani wa chama cha CCM, Abdulrahman Kinana amepewa onyo na kutokugombea  nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 18 huku katibu Mkuu wa zamani, Yusuf Makamba akisamehewa.


Polepole alikuwa akieleza uamuzi wa kamati kuu ambayo ilitoa siku saba kwa kamati ya nidhamu iliyowahoji vigogo hao kukamilisha suala lao na kuwasilisha taarifa.

Kinana, Makamba pamoja na Membe walihojiwa kwa nyakati tofauti Dodoma na  jijini Dar es Salaam kutokana na kutuhumiwa kwa makosa ya kimaadili.

Agizo la viongozi hao kuhojiwa lilitolewa na Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana Mwanza, Desemba 13, 2019.

========  ========  ======

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemvua uanachama Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe, huku Katibu Mkuu mstaafu Abdulrahman Kinana akipewa karipio na kutakiwa kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 18 na Katibu Mkuu mwingine mstaafu Yusuf Makamba akisamehewa.

Hayo ameyasema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Tafia (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole jijini Dar es Salaam leo. amesema, CCM imechukua hatua hizo kupitia maamuzi ya Kikao Cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika, Katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.

Kabla ya Kikao cha Kamati Kuu (CCM) cha leo, hivi karibu Kamati Kuu hiyo ilifanya kikao ambapo pamoja na mambo mengine ilitoa siku saba kwa Kamati Ndogo ya Nidhamu na Maadili iliyowahoji Kina Kinana, Membe na Makamba kukamilisha taarifa na kuwasilisha kwenye vikao vitakavyofuatia.

Walikuwa tayari wameshahojiwa na Kamati hiyo kwa nyakati tofauti ambapo Membe alihojiwa jijini Dodoma na Kinana na Mzee Makamba walihojiwa jijini Dar es Salaam kutokana na tuhuma za makosa ya kimaadili.

Agizo la kuhojiwa Kina Membe, Kinana na Mzee Makamba, lilitolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Kikao chake kilichofanyika jijini Mwanza, Desemba 13, 2019.

Viongozi hao wastaafu waliingia matatani baada ya sauti zao kusambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wakieleza mambo mbalimbali na madai ya chama kushindwa kuwalinda Makatibu Wakuu hao wastaafu dhidi ya mtu anayejiita mwanaharakati, ambaye alisambaza sauti hizo na akitoa tuhuma dhidi yao.

 “Uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonyesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo.” amesema Polepole akizungumzia kuhusu adhabu aliyopewa Membe

Amesema Kamati Kuu imepokea maelezo ya Kinana na baada ya kuyatafakari kwa kina ndipo imeazimia apewe adhabu ya karipio kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili za chama hicho toleo la 2017.

“Adhabu ndani ya CCM kuna za siri ambazo ataambiwa mhusika na zinaweza kuwa za wazi. Adhabu ya karipio na kufukuzwa zinasomwa hadharani.

Adhabu ya karipio imeanishwa katika kanuni na inasema, "mwanachama anayefanya kosa linalokipaka matope chama na bila kuonyesha nia ya kujirekebisha basi kamati kuu inaweza kumpa mwanachama huyo adhabu ya karipio.”

“Mwanachama aliyepewa adhabu ya karipio atakuwa katika hali ya matazamio kwa muda usiopungua miezi 18 kutoka tarehe ya leo (Februari 28, 2020) ili kumsaidia mwanachama huyu katika jitihada za kujirekebisha. Akiwa katika kipindi hicho hatakuwa na haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika chama lakini atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wa chama kama ana dhamana hiyo.” Amesema Polepole

Kuhusu Makamba amesema Polepole amesema, baada ya fuatilia, kumhoji na kufuatilia mwenendo wake, Kamati Kuu imeazimia kwa kauli moja kwamba Makamba asamehewe makosa yake aliyotenda.

“Imetoa msamaha huu kwa misingi kuwa Makamba wakati wote tangu aliposomewa mashtaka yake amekuwa mtu muungwana, mnyenyekevu na mtii kwa mamlaka ya chama. Kubwa kuliko yote ameomba asamehewe makosa yake kwa barua zilizoambatanishwa katika maelezo yake. Amesamehewa makosa yake.” amesema Polepole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...