Naibu Waziri wa Kilimo.na Mifugo Abdallah Hamis Ulega akizungumza katika mkutano wa siku moja wawataalam wa mifugo na Watafiti katika ukumbi wa Mauntmeru Holel leo.

Na.Vero Ignatus,Arusha

Serikali kupitia wizara ya mfugo imepokea utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha kilimo Sokoine kwa kushirikiana na chuo cha Livepol cha Uingereza na kile Bristone uingereza kuhusu athari na njia za kudhibiti magonjwa ya minyoo

Utafiti huo pia uliangazia kuwepo kwa sugu wa vimelea vya magonjwa hayo kwa dawa zinazotumika kuua minyoo hiyo kwa sasa ambapo kwa sehemu kubwa hushambulia kwenye ini la mnyama

 Naibu waziri wa Wizara ya Kilimo na Mifugo  Hamisi Abdalla Ulega katika  mkutano wa wataalamu wa mifugo magonjwa yatokanayo na minyoo Bapa yanaonekana kupunguza uzalishaji kwa 10%

Ulega alisema  serikali imekuwa na mikakati na jitihada mbalimbali kupambana na magonjwa ya mifugo ikiwemo kugawa dawa za kuogeshea mifugo nchi nzima na kuzalisha chanjo za magonjwa ya msingi kwa lengo la kukuza uzalishaji.

Aidha amesema kuwa serikali inaahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yatakayotolewa na utafiti huo ili kuhakikisha magonjwa hayo ya minyoo yanatokomezwa nchini.

Kwa upande wake Profesa Hezron Nonga Mkurugenzi wa huduma za mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi alisema kuwa mwaka wa fedha 2019/20 serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 450 kwaajili ya kununua lita 12,550 kwaajili ya majosho 1733 kwa nchi nzima.

Sambamba na hayo amewataka wafugaji kuwa na kuwaogesha wanyama mara mbili kwa mwezi ili kuwa na wanyama wenye nguvu  na afya.
Washiriki wa mkutano huo
Katikati ni Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Abdallah Hamis Ulega kushoto kwake ni Profesa  Hezron Nonga Mkurugenzi wa huduma za mifugo Wizara ya Mifugo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...