Msajili wa Baraza la Famasi Elizabeth Shekhalage akikagua moja ya stoo ya dawa kwenye hospitali.
Mfamasia kutoka kitengo cha huduma za dawa, wizara ya afya Daniel Pyuza akikagua moja ya stoo kwenye ziara ya katibu mkuu wa wizara hiyo

……………………………………………..

Na. Catherine Sungura-Kasulu.


Wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini wametakiwa kuhuwisha leseni zao kila mwaka.

Hayo yamesemwa na msajili wa baraza la wafamasia kutoka wiza ya afya Elizabeth Shekhalage wakati akiongea na watumishi wa hospitali ya halmashauri ya mji Kasulu kwenye ziara ya katibu mkuu wa wizara ya afya

Msajili amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mabaraza ya kitaaluma,kila anayestahili kuwa na leseni ni wajibu wake kuzingatia takwa hilo na hivyo kutimiza kwa mustakabari wa taaluma zao

“Kila mwaka mnatakiwa kutoka kwenye gazeti la serikali,hakikisheni wote mna leseni ili mtimize takwa la kisheria”.Alisisitiza Shekhalage.

Kwa upande mwingine Shekhalage aliwataka watumishi wa afya wenye maduka ya dawa,wawe na maduka ya mfano kwa kusajiliwa kwani hakuna kifungu kinacho wazuia wasiwe nayo.

Aidha, aliwataka watumishi hao kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi holela ya dawa ambayo husababisha usugu wa vimelea vya dawa kwa binadamu.

“Matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kutumia dawa bila.kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na wataalam au kutotunza dawa vizuri husababisha athari nyingi kwa binadamu ikiwemo kuongezeka kwa ugonjwa ama madhara yasiyo ya lazima kwa wagonjwa”.Alisisitiza

Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kununua dawa bila kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kupara vipimo na kupata ushauri kutoka kwa wataalam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...