Mkandarasi anayejenga barabara yenye urefu wa kilomita 1.2 kutoka Daraja la Nyerere hadi Feri – Kibada ametii agizo la Rais John Magufuli la kumtaka kuanza kazi ya kukamilisha mradi huo haraka.

 China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) jana ilianza kazi ya kutengeneza kipande cha barabara hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la kumaliza mgogoro wa kikandarasu na kukamilishaa mradi huo.
Akizugumza wakati wa uzinduzi wa ofisi za Wilaya ya Kigamboni,. Rais Magufuli alieleza kutoridhishwa kwake na ucheleweshaji wa mradi huo kutokana na suala la gharama.
Katikaa taarifa kwa vyombo vya habari jana, CRCEG ilisema:  “Tunataka kutoa shukrani zetu za dhati na kuunga mkono ari ya ‘Hapa Kazi Tu’ and ‘Utii wa Sheria’ unaotiliwa mkazo na Mheshimishwa Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukamilisha mradi huu kwa kiwango cha daraja la juu na gharama nafuu bila kuchelewa.”
Mkandarasi huyo ameeleza kuwa mradi ulichelewa, pamoja na mengine, kutokana na kuchelewa kukabidhiwa eneo la mradi kutokana na nyumba zilizopo, makaburi na majengo mengine yaliyokuwepo ndani ya eneo la barabara. Malipo ya fidia yalikamilika mwishoni mwa Mei 2018.
Kuchelewa kwa mwajiri (NSSF) kumteua meneja mpya wa mradi ni sababu nyingine ya kuchelewa kuanza kazi hiyo, kwa mujibu wa mkandarasi.  Wakati ambapo mameneja wa awali walisimamisha uangalizi wa kazi hiyo Mei 1, 2019, meneja mpya aliteuliwa wiki iliyopita.
“Ni tarehe 14 Februari tu ndipo mwajiri alimjulisha mkandarasi kuhusu wa kuletewa Tanroad kama meneja mpya wa mradi ambaye anaanza kazi tarehe 17 Februari (jana),” ilisema taarifa ya CRCEG.
Sababu nyingine za kuchelewa kwa mradi huo, kwa mujibu wa mkandarasi, ni kuchelewa kwa malipo kwa muda mrefu na kusababisha kukwama kwa mtiririko wa fedha kwa mkandarasi, pamoja na kuchelewa kwa idhini ya kuhamisha wananchi katika makazi mapya na utunzani wa miundombinu iliyokuwepo katika eneo la mradi, kama vile Bomba la Mafuta la TAZAMA, Bomba la Mafuta la MOIL na Bomba la Kusambaza Maji la TIPER.
Ucheleweshaji wa gharama za kuhamisha nyaya za umeme za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ilitajwa kama sababu nyingine ya kuchelewa kwa mradi huo.

Wakati huo huo, CRCEG imeeleza kuwa sababu ya kuongezeka kwa gharama za mradi ni pamoja na ukweli kwamba barabara hiyo inajengwa kwa ubora wa hali ya juu ikiwa ni kiwango cha barabara za Haraka (Express) ambacho ni kiwango cha juu zaidi hapa nchini.

Mkandarasi huyo alieleza kuwa gharama pia ilikuwa juu kwa kuwa maeneo kadhaa yaliathiriwa na mabaki ya mafuta, na hivyo kulazimika kufanyika kwa uchimbuaji wa kwenda chini kujazia udongo ulioathiriwa na mafuta.

CRCEG imeeleza pia kuwa barabara inapita katika maeneo yenye topetope yanayohitaji uchimbuaji kuondoa udongo na kujaza kama njia ya kuimarisha ufanisi wa kimakanika.

Kulikuwa pia na gharama za ziada za kuhamisha makazi ya watu na utunzaji wa miundombinu kwa huduma ambazo zilikuwa ndani ya eneo la mradi, ambavyo vyoye vinaidhinishwa na mwajiri.

Mkandarasi pia amemshutumu mwajiri kwa kuchelewesha malipo, na hivyo kusababisha kuongezeka kwa riba “bila sababu’. 

Pia kulikuwa na uchimbuaji wa kuondoa udongo wenye ogani na kujaza udongo usio na ogani, na pia kazi za kazi za upimaji wa marudio wa kiasi halisi kwenye eneo la mradi, yaani mfumo wa mifereji ya maji ambao awali haukuzingatiwa kwenye tathmini.

Mradi huo ulisimamishwa tarehe 31 Desemba 2018 kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Meneja Mradi, wakati ukisubirishwa utatuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo uidhinishaji wa vitu vya ziada na mwajiri. “Uidhinishaji huo haujafanyika hadi sasa,” kwa mujibu wa mkandarasi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka kampuni ya CRCEG, David Zhou (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu utayari wa kampuni hiyo kumalizia ujenzi wa barabara ya Feri- Kibada inayonganisha na daraja la Nyerere wilayani Kigamboni kulingana na agizo la Rais John Magufuli sambamba na kuelezea sababu za kuchelewa kwa utekelezwaji wa mradi huo. 
Meneja wa Miradi wa barabara ya Feri- Kibada inayounganisha na daraja la Nyerere Wilayani Kigamboni, Muhandisi Jamal Mruma kutoka kampuni ya CRCEG (mbele kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari vifaa vya ujenzi vinavyotumika kwenye mradi huo wakati akieleza utayari wa kampuni hiyo kumalizia ujenzi wa barabra hiyo kuanzia jana kulingana na agizo la Rais John Magufuli sambamba na kuelezea sababu za kuchelewa kwa utekelezwaji wa mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...