
Mkuu wa shule ya Sekondari ya
Canosa sister Irine Nakamanya akipokea cheti cha pongezi kwa shule hiyo
kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne na pili.


Wanafunzi na walimu waliokuwa
katika hafla ya kupongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato
cha nne na cha pili mwaka 2019. Hafla hiyo imeandaliwa na Idara ya elimu
Sekondari.


Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Hamis Lissu katikati mwenye suti nyeusi, akiwa na Afisa Elimu
Sekondari wa Halmashauri ya Kinondoni ,Leornad Msigwa wa kwanza kushoto
na Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa Bi. Maimuna Matanda wakati wa hafla ya
kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya
kidato cha nne na pili.
*****************************
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha
nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa
Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Hamis Lissu wakati wa hafla ya
utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri kwa matokeo hayo
kitaifa na kimkoa kwa mwaka 2019 /2020.
Lissu amesema kuwa Halmashauri
hiyo imekuwa ikifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa kila eneo ikiwemo
Elimu, Afya na mazingira, Michezo na maeneo mengine na kusema kuwa
mafanikio hayo yanatokana na kuwa na Mkurugenzi mwenye juhudi za kufanya
kazi inayoendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na
Dk. John Pombe Magufuli.
Lissi amefafanua kuwa Mkoa wa Dar
es Salaam unajumla ya Halmashauri tano lakini Halmashauri ya Kinondoni
inayo ongozwa na Mkurugenzi wake Aron Kagurumjuli imekuwa ikifanya
vizuri katika sekta ya elimu ambapo imeongoza kuwa na matokeo mazuri kwa
miaka minne mfululizo katika mkoa huo.
” Kinondoni imekuwa ikifanya
vizuri sana kwenye mambo mengi, binafsi mnanikosha na utendaji wenu
uliotukuka ,niwasihi nguvu hii mliyokuwa nayo muendelee nayo ili
kuendelea kuwa na rekodi nzuri kwa kuwa mfano bora kwa Halmashauri
nyingine zilizopo katika mkoa wetu” amesema Bwana Lissu.
Lakini pongezi hizi pia zimuendee
zaidi Mkurugenzi Kagurumjuli, Kinondoni mmepata Mkurugenzi bora,
anafanya vizuri sana kwenye Halmashauri yake,na uchapakazi huu ndio
anaoutaka Mhe. Rais wetu Dk. Magufuli, tukiwa na wachakazi kama hawa,
hakika kwenye mkoa wetu tutakuwa na matokeo makubwa zaidi kwenye kila
eneo” ameongeza Bwana Lissu.
Kwa upande wake Afisa Elimu
Sekondari, wa Halmashauri hiyo, Bwana Leornad Msigwa amesema katika
matokeo ya kidato cha nne Kinondoni ilishika nafasi ya 39 kati ya
Halmashauri 195 na hivyo kufanya kupanda nafasi tatu kitaifa
ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilishika nafasi ya 42 na kuendelea
kuongoza kwa kishindo kwa miaka mine mfufulizo katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Msigwa ameongeza kuwa tathmini ya
matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2019 inaonyesha kuwa ufaulu
umeongezeka kwa silimia 0.59 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ufaulu
umekuwa kwa asilimia 81.21 ambapo mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa
asilimia 81.80.
Kwa upande wa matokeo ya kidato
cha pili , Msigwa ameeleza kuwa tathmini ya upimaji wa matokeo ya
kidato cha pili kwa mwaka 2019 , ufaulu ulikuwa kwa silimia 94.04 na
hivyo kufanya Halmashauri ya Kinondoni kushika nafasi ya 24 kitaifa kati
ya Halmashauri 184 na hivyo kupanda nafasi 10 kitaifa ukilinganisha na
mwaka 2018.
Msigwa amefafanua kuwa, katika
matokeo hayo mwaka 2019 watahiniwa walikuwa 9,340 ambapo waliofaulu
mtihani huo kati ya daraja 1-1V walikuwa 8,783 sawa na asilimia 94.04.
Amefafanua kuwa kati yao waliopata
alama za ufaulu wa daraja la kwanza ni 1,682, daraja la piIi ni
1,216, daraja la tatu 1,556, daraja la nne 4,329 huku jumla ya
watahiniwa 557 walipata alama ya sifuri.
Katika hatua nyingine Msigwa
amewaeleza walimu wa shule za Sekondari waliokuwa katika hafla hiyo
kuendelea kujituma zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ili
kuwezesha Halmashauri hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa na
kimkoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...