Na Woinde Shizza, Arusha
Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo ametoa wito kwa watalii duniani kote kuendelea kutembelea vivutio vyetu hata katika mwaka huu Wa uchaguzi kwani nchi yetu ina ulinzi wa kutosha na amani .
Aliyasema hayo jana katika sherehe za kuadhimisha miaka 43 ya chama cha mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid ambapo aliwatoa hofu wataliii wote wanaokuja kutembelea vivutio hapa nchini na kusema kuwa nchi yetu ina amani na ulinzi Wa kutosha.
Alisem kuwa serikali inaendelea kuimarisha ulinzi Na usalama Wa uhakika ili watalii waendelee kuja kwa wingi na utalii wetu uweze kukuwa kwa kasi ,huku akibainisha kuwa japo kuwa ni mwaka Wa uchaguzi nchi yetu bado itakuwa na usalama Wa kutosha .
"Nchi yetu ni nchi ya amani hivyo napenda kuwasihi watalii wetu wasiache kuja wakiofia ni mwaka Wa uchaguzi hivyo kutakuwa na fujo niwatoe hofu kwa hilo kabisa usalama wetu ni mzuri ma kadri siku zinavyozidi kwenda unazidi kuboreshwa " alibainisha gambo
Alobainisha kuwa kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wanaponda ujio Wa ndege zetu na kudai kuwa hazina faida ambapo alibainisha kuwa tangu kija kwa ndege zetu uchumi unakuwa katika sekta ya utalii kwani ndege zile zinatumika pia kutangaza vivutio vyetu
"Iwapo ndege labda ikitua China au Dubai MTU akiona ile ndege imeandikwa ngorongoro kwanza atataka kujua nini na pale Ambapo ataambiwa nini atataka kujua imetoka nchi gani akijua atataka kujua hapo tayari kabisa tunakuwa tumeshaitangaza nchi yetu na vivutio vyetu" alibainisha hivyo Gambo
Alisem kuwa tangu kuja kwa ndege hizo kumekuwa na ushinda mkubwa uliosabisha hata Yale makampuni ambayo walikuwa wanafanyakazi kwa kujisikia ,au bei zao za ndege zipo juu wanapunguza hivyo ni vyema kila mtanzani kupenda cha nyumbani.
Kwa upande upande wake Katibu Wa NEC Siasa na ushirikiano Wa kimataifa kanali mstaafu Ngemela Lubinga aliwataka wananchi kusaidiana na vyombo vya ulinzi na usalama kulinda usalama Wa Arusha na nchi yetu kwa ujumla .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...