Wadau wote kupitia vyama vyao waitwa kuleta mapendekezo ili kuboresha sekta zao ikiwa Serikali ipo kwenye maandalizi ya bajeti ukizingatia pia Wizara ya Viwanda na Biashara inatekeleza mpango kazi wa Blue Print ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Mhe Stella Manyanya alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa umoja wa wazalishaji na wasindikaji wa  muhogo Tanzania (TACAPPA) katika mkutano wa wadau wa muhogo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam. 

 “Tozo zipatazo 114 ziliondolewa kwa mwaka 2017/2019, tozo 5 zimeondolewa mwaka 2018/2019 na tozo 54 zimeondolewa kwa mwaka 2019/2020 ikiwemo kuhamisha jukumu la usimamizi wa ubora wa chakula kutoka TFDA kwenda TBS” amesema Mhe Manyanya

Amezielekeza taasisi zake kushirikiana ili kutoa mafunzo ya usindikaji kwa wazalishaji, alama ya ubora wa bidhaa, kubuni teknolojia rahisi na kuwatafutia masoko ikiwa ni wakati muafaka wa kuwekeza katika mnyororo wa thamani wa zao la muhogo 

Nae, Mwenyekiti wa Umoja huo Bi Mwantumu Mahiza ameeleza kuwa umoja upo kwenye hatua ya kukamilisha andiko kwenda Serikali za mitaa ili shule za sekondari za bweni zilime mihogo kwaajili ya mahitaji ya chakula, kuwajenga elimu na maarifa ya kilimo bora cha muhogo kwa vijana ili waweze kujitegemea.  

TanTrade imesmamia uanzishwaji na usajili wa Chama cha Wazalishaji na Wasindikaji wa Muhogo Tanzania, lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo.  

 Mhandishi Mhe Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  akiangalia bidhaa iliyoongezwa thamani kutoka kwa mkulima wa zao la muhogo  alipofunga mkutano wa umoja wa wazalishaji na wasindikaji wa muhogo Tanzania
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akielezea namna Mkoa wa Tanga ulivyoweka mikakati ya kuinua zao la muhogo na kuwa la kibiashara na sio chakula pekee katika mkutano wa wazalishaji na wasindikaji wa muhogo Tanzania uliofanyika katika ofisi za TanTrade
  Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka akiongea na wadau walioshiriki kwenye mkutano wa wazalishaji na wasindikaji wa zao la muhogo Tanzania ambapo TanTrade imekuwa msimamizi wa uanzsihaji wa umoja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...