Na Mwandishi Wetu Katavi

Msafara wa kijinsia unaolenga kutokomeza vitendo vya kikatili kuelekea Siku ya Wanawake Duniani umezinduliwa rasmi mkoani Katavi.

Akizungumza wakati akizindua Msafara huo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera amesema kuwa vitendo vya kikatili vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii zetu hivyo vinatakiwa kupatiwa mbinu ya kupambana navyo.

Ameongeza kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona wanawake na watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili hivyo itahakikisha inazishugulikia kesi zote za vitendo vya ukatili.

"Sheria ifuate mkondo hata mimi naweza kutelekezwa na hata mimi nikitelekeza nikamatwe tu" alisema

Mhe. Homera amesisitiza vyombo vya Sheria na Taasisi zisizo za Kiserikali kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanapata mbinu stahiki itakayosaidia kuondokana na vitendo vya ukatili.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bi. Imelda Kamugisha amesema lengo la msafara huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili na namna ya kupambana na vitendo hivyo kuelekea maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.

"Msafara huu umelenga kutoa elimu kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kuendeleza jitihada za Serikali na wadau katika kuhakikisha tunaondokana na vitendo vya kikatili" alisema

Naye Nurdin Bilal Maarufu Shetta amesema wasanii wameungana na Serikali katika kusambaza elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili ili kuwezesha kuondokana na vitendo hivyo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.

"Tuko tayari na tumeamua wasanii kuingia katika haya mapambano muhimu ya kitaifa dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii Caren Mitta kuhusu utaoji wa huduma za Ustawi wa jamii katika Msafara huo uliozinduliwa leo mkoani Katavi.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Katavi na wasanii mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia leo mkoani humo.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akieleza lengo la msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili uliozinduliwa leo Mkoani Katavi.
 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na wananchi wa Wilaya Mpanda wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia leo mkoani humo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta akitumbuzia wanafunzi wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkaoni Katavi.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiagana na Msanii Shetta mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkoani Katavi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...