Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha kutoa ratiba ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, na kuwataka wananchi kupuuza taarifa inayosambaa kwenye mitandao kwani si taarifa rasmi na imeandaliwa kwa nia ovu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo Dkt. Wilson Charles inaeleza kuwa taarifa hiyo potofu inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii hasa WhatsApp.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kujibu wa Ibara ya 74(6)(b) na (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imepewa mamlaka ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Katika kutekeleza jukumu hilo, kifungu cha 35B cha Sheria ya Uchaguzi, sura ya 292, kinaipa NEC mamlaka ya kutangaza katika gazeti la Serikali tarehe ya Uchanguzi” alisema Dkt. Charles.

Aliongeza kuwa, mamlaka hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(1) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinailekeza NEC kutangaza tarehe ya uchaguzi mara baada ya Bunge kuvunjwa. 

Aidha, kwa kuwa Bunge halijavunjwa, NEC haijatoa wala kutangaza ratiba yoyote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Mwisho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...