Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

WAKURUGENZI watatu wa Kampuni ya Civmark Ltd na Wakili wa kujitegeme wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ya kughushi mkataba kwa lengo la kupata zabuni ya kujenga barabara ya Manispaa ya Bukoba kwa kiwango cha lami.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Adolf Lema
amewataja washitakiwa hao kuwa ni Crispin Mwombeki na mke wake Hadija Nyumbwe, Joseph Nyamwero na Wakili Glory Benne.

Mbele ya Hakimu Mkazi Rashid Chaungu imedaiwa Septemba 17, 2017 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Mwombeki na Nyamwero kwa nia ya kudanganya walighushi mkataba wa makubaliano ya pamoja kuonesha kuwa kampuni  ya Civmark Ltd na Mecco Ltd zimekubaliana kuunda mkataba huo kwa jina la Cvmark Mecco Jv kwa lengo la kupata zabuni ya kujenga barabara ya Rubya-Kanyamabogo huku wakijua kuwa siyo kweli.pa

Katika shtka la pili imedaiwa, Septemba 20,2017 jijini Dar es Salaam, washitakiwa Mwombeki, Nyumbwe na Benne kwa nia ya kudanganya walighushi nguvu ya uwakilishi wa kisheria kuonesha kampuni hizo zimekubaliana kutoa nguvu ya uwakilishi wa kisheria kwa Nyamwero kuwawakilisha kwenye zabuni hiyo.

Aidha Oktoba 10, 2017 maeneo ya Bukoba mkoani Kagera, mshtakiwa Mwombeki alighushi nyaraka kuonesha kampuni ya Mecco imekubali kutoa nguvu ya uwakilishi wa kisheria kwa Nyamwero kuiwakilisha kampuni katika zabuni ya ujenzi wa barabara ya Manispaa ya Bukoba kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilometa tano.

Imeendelea kudaiwa kuwa Mwombeki alighushi pia nyaraka kuonesha kuwa kampuni ya Mecco Ltd ina uwezo wa kutengeneza barabara ya Manispaa hiyo kwa kiwango cha lami.

Hata hivyo, washitakiwa wote wamekana kutenda mashtaka hayo na upande wa mashitaka umeieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba hawana pingamizi na dhamana endapo washtakiwa watakidhi masharti.

Wakili wa Utetezi, Paschal Kamala aliiomba mahakama hiyo iwape wateja wake masharti nafuu ya dhamana kwa sababu kwa miaka mitatu wamekuwa wakiripoti polisi bila kukosa.

Akisoma masharti ya dhamana Hakimu Chaungu amemtaka kila mshitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa, nakala ya kitambulisho na kusaini Bondi ya Sh milioni tano.

Washitakiwa wote  wametimiza masharti na wameachiwa kwa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26, mwaka huu kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashitaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...