Na Chalila Kubuda, Globu ya Jamii .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza muda wa uandikishaji katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa ya Dar es Salaam.

Muda uliongezwa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura ni siku tatu ambapo zoezi hilo litaitimishwa Februari 23, 2020.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchanguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles amesema kuwa kusogezwa kwa zoezi hilo kumetokana na maombi mbalimbali katika vituo vya uandikishaji.

Dkt.Charles amesema baada ya maombi hayo walifanya kikao cha Februari 19 kwa ajili ya kutathmini zoezi hilo na kuamua kuongeza muda wa kujiandikisha. Amesema vituo vyote vitafunguliwa kama kawaida kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.

Aidha amesema NEC inawasihi Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutumia vizuri muda ulioongezwa kuhakikisha taarifa zao zinaingizwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwani hakuna muda mwingine wa nyongeza katika awamu ya Kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu.

Kauli mbiu ya uandikishaji kwa Daftari la kudumu la Wapiga kura  ni "Kadi yako,Nenda Kajiandikishe'

 Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Charles akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari kuhusiana na kuongeza muda wa siku tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura kwa mkoa wa Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Charles akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kuongeza muda wa siku tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura kwa mkoa wa Dar es Salaam.Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...