
Kamati hiyo imeeleza kuwa viongozi hao wamekuwa wanatoa maneno ya kukashifu na kudhalilisha viongozi ,Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti tofauti.
Wamesema viongozi na Makocha waliobainika ni wafuatao Kocha wa Klabu ya Namungo FC(Hitimana )-kwenye mchezo wa Simba SC na Namungo Fc, Kocha wa Klabu ya Young African Sc (Luc Aymael)-kwenye mchezo wa Yanga Sc na Lipuli.
Wengine ni Msemaji wa Klabu ya Simba SC (Haji Manara) na Muhamasishaji wa Young African sc(Anthonio Nugaz) .
Kutokana na matamshi hayo wanapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...