Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MSHINDI wa BSS mwaka 2019, Meshack Fukuta amesema kuwa akipata hela zake za ushindi ambazo ni shilingi Milioni 20 atazitumia kwa ajili ya muziki wake na  sio kula bata kama watu ambavyo wamezoea.

Akizungumza na Michuzi Tv amesema kuwa hela ambazo anazitegemea kuzipata hivi karibu sio ndogo wala sio nyingi ila asipo tuliza akili anaweza kuja kujikuta amezitumia bila ya kutimiza malengo yake.

“Sijapata hela bado na ni lazima nijipange ili nisije kuchanganyikiwa naogopa sana kushindwa kuja kufanya vizuri fedha hizo nitazitumia kwa ajili ya muziki wangu na wala sina mpango wa kula bata ," Ameeleza

Amesema  kuwa licha ya BSS na wao kuwekeza shilingi Milioni 30 kupitia muziki wake kama mkataba wao unavyoeleza ila na yeye ameona ni bora kuwekeza na hizo hela kwa ajili ya muziki ili kuweza kutimiza malengo yake.

Pia amewaasa vijana ambao wana vipaji kutokata tamaa na kufanya jitihada ili waweze kufika mbali kupitia vipaji vyao.

Aidha amesema kuwa BSS ni moja ya taasisi ambayo takribani miaka 10 sasa imeendelea kusaidia vijana wenye ndoto za kuwa  wanamuziki wakubwa na wenye majina hivyo ni jukumu la vijana kufanya jitihada ili watu waweze kuona kipaji vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...