Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MBUNGE wa Kigoma mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amechukua fomu ya kugombea nafasi ya kutetea kiti cha uongozi wa  Chama cha ACT Wazalendo kwa mhula wa pili na wa mwisho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu.
 
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya  kuchukua fomu hiyo muda mfupi  baada ya kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili ambapo katika shauri hilo la uchochezi amekutwa na kesi ya kujibu Zitto amesema;
 ameamua kutetea nafasi hiyo kwa awamu ya pili kama katiba ya ACT Wazalendo inavyoeleza na hiyo ni baada ya kushauriana na watu mbalimbali wakiwemo viongozi na  familia yake.
 “Nimechukua fomu ya kugombea tena nafasi ya uongozi wa chama katika uchaguzi utakaofanyika katika mkutano wa chama utakaoanza Machi 14 hadi 16, mwaka huu.” Ameeleza.

Amesema kuwa tayari ametumikia  muhula mmoja na kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo mihula ya uongozi ni miwili, na kueleza kuwa muhula huo wa pili ni wa mwisho kwa mujibu wa katiba ya ACT Wazalendo.

Aidha Zitto amewashauri wanachama kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama kwa kuwa hakuna nafasi ya mtu hivyo ni haki ya kila mwanachama  kugombea na kupata ridhaa kutoka kwa wanachama ili kujenga demokrasia ya nchi.

Kwa upande wake katibu, kampeni na chaguzi taifa Mohammed Massaga amesema kuwa hadi sasa wanachama 58 wameomba na kuchukua  fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...