Na Amiri Kilagalila, Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ametoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji,maafisa elimu kata pamoja na viongozi wa mitaa na vijiji kuhakikisha wanafunzi 708 ambao hawajajiunga na masomo ya kidato cha kwanza,vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Sendeka ameonyesha Kukasirishwa na kitendo cha wanafunzi hao 708 waliofaulu kidato cha kwanza na kushindwa kujiunga na masomo.
Ametoa agizo hilo katika kikao cha tathimini ya elimu kilichowakutanisha halmashauri zote za mkoa huo na wadau wa elimu ambapo amesema ni jambo la kushangaza kuona wanafunzi wanagoma kuendelea na masomo wakati serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuboresha miundombinu ya elimu hivyo zoezi la kuwatafuta na kuwapeleka shule wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza.
"Nichukue nafasi hii kuwaelekeza wakuu wangu wa wilaya,wakulugenzi watoto wote ambao hawajaripotikidato cha kwanza,natoa mwezi mmoja kutoka leo,yeyote ambaye atakuwa hajaripoti baada ya hapo watendaji wa kata husika,maafisa elimu,viongozi wa vijiji husika wachukulieni hatua,simamieni ninyi wenyewe na maafisa elimu wenu"alisema Ole Sendeka
Akiweka bayana kuhusu idadi ya wanafunzi waliofauru kidato cha kwanza, walioripoti na ambao hawajaripoti tangu januari 6 shule zilipofungua ,afisa elimu mkoa wa Njombe Gift Kyando anasema takribani wafunzi 15,711 walifauru lakini asilimia 84.7 pekee ndiyo walioripoti shule na kuitaja wilaya ya Ludewa kuwa na wanafunzi 200 ambao hawajaripoti.
"Kwanza lengo kubwa kwenye mkutano huu ilikuwa ni kuangalia wapi tumetoka na tukaolekea pamoja na mstakabali mzima wa elimu,hali ya kuripoti wananfunzi katika shule zetu waliomaliza mwaka 2019 na kujiunga kidato cha kwanza 2020 si mbaya sana lakini bado kuna wanafunzi ambao hawajaripoti na mpaka sasa ambao hawajaripoti ni 708"alisema Gift Kyando
Nao baadhi ya wadau wa elimu wakitoa mapendekezo ya kuboresha sekta ya elimu akiwemo Flaten Kwahison, Ewdin Mwanzinga na Joram Hongoli mbunge wa Lupembe wanasema ili mkoa uweze kupiga hatua inapaswa kuboresha mazingira ya kupokea na kutoa elimu ,nidhamu na umoja ambayo utekelezaji wake utafanyika kimkakati wa mda mfupi na mrefu.
Katika kikao hicho tuzo za fedha na vyeti zimetolewa kwa halmashauri na shule ambazo zimefanya vizuri kitaaluma.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akitoa maelekezo
ya kuwafikisha wanafunzi 708 ambao hawajaripoti shule,katika kikao cha
tathmini ya elimu kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa
Njombe.
Afisa elimu mkoa wa Njombe Gift Kyando akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kikao cha tathmini ya elimu kilichofanyika mjini
Njombe.
Flaten Kwahison mmoja wa wajumbe na wadau wa elimu mkoani Njombe
akichangia hoja namna ya kuboresha kiwango cha elimu mkoani humo.
Baadhi ya wajumbe katika kikao cha tathmini ya elimu mkoani Njombe
wakisikiliza michango ya wadau wa elimu walikotoka kama mkoa wa Njombe
na namna ya kuboresha zaidi katika swala la taluma.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka na baadhi ya viongozi wa
halmashauri ya mji wa Njombe akiwemo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Njombe Iluminatha Mwenda walipokabidhiwa zawadi ya kombe kwa Kutokana
na halmashauri ya mji wa Njombe kushika nafasi ya sita kitaifa kati ya
halmashauri sita nchini zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha
nne
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...