Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda na Uganda wametia saini makubaliano ya kukabidhiana wahalifu wanaosakwa na nchi hizo.

Makubaliano hayo yametiwa saini katika mkutano uliofanyika katika mpaka ukisimamiwa na Marais Paul Kagame na Yoweri Museveni.

Mkutano huo uliunga mkono kuachiliwa kwa makumi ya raia waliokuwa wakizuiliwa kutoka pande zote mbili katika kipindi cha wiki chache zilizopita.

Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwahifadhi waasi wanaokabiliana na serikali ya taifa hilo huku Uganda ikimlaumu jirani yake wa kusini kuingilia vikosi vyake vya usalama.

Uganda sasa imekubali kuchunguza na kubaini madai ya Rwanda kwamba waaasi wa Rwanda wamekuwa wakisajili na kufanya mafunzo ndani ya Uganda. Pia imekubali kuzuia tatizo kama hilo kufanyika tena ndani ya ardhi yake.

Hali ya wasiwasi kati ya viongozi hao wawili inaonekana kupungua. Rais Paul Kagame na Yoweri Museveni walionekana wakisaliamana na kupeana mikono huku wakitabasamu wakati walipowasili kwa mkutano huo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...