Waziri Mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane,  alikosa kufika mahakamani siku ya Ijumaa kwa ajili ya kesi ya mauaji inayomuandama, kutokana na kile kilichotajwa na familia yake kama sababu za kiafya. Polisi ya nchi hiyo siku ya Alkhamisi ilisema kiongozi huyo angeshtakiwa rasmi jana Ijumaa kwa mauaji ya mke wake wa zamani.

Potlako Thabane, mtoto wa kiume wa Thabane amesema Waziri Mkuu huyo amepelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu, na wala hajakimbia nchi na mashitaka yanayomkabili kama inavyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Naibu Kamishna wa Polisi, Paseka Mokete amesema iwapo Waziri Mkuu huyo atajaribu kukimbia mkono wa sheria, basi vyombo vya usalama vitatoa waranti ya kumkamata. Waziri Mkuu huyo wa Lesotho tayari ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake huo.

Mke wa zamani wa Waziri Mkuu huyo wa Lesotho, Lipolelo Thabane, 58, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake mnamo Juni 14 mwaka 2017 alipokuwa anarudi nyumbani huko Maseru, mji mkuu wa Lesotho.

Siku mbili baadaye, mumewe, Thomas Thabane aliteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Lesotho. Kabla ya Lipolelo kuuawa hapo mwaka 2017, mke huyo wa zamani wa Waziri Mkuu wa Lesotho na mumuwe walikuwa katika mchakato wa kutalikiana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...