Dar es Salaam. Shabiki wa timu bingwa kihistoria ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Mohamed Ngolo ameshinda sh 166,397.840 kupitia droo ya kwanza ya mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.

Ngolo ambaye fundi katika mkoa wa Manyara ameweza kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani na kuwa mshindi wa kwanza wa droo ya Perfect 12 mwaka huu.

Meneja Masoko wa kampuni ya M-BET, Allen Mushi alisema kuwa wamerafirijika kupata mshindi wa kwanza mwaka huu kuibuka na mamilioni ya fedha.

Mushi alisema kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa na wataaendelea kutoa washindi wengi zaidi mpaka mwishoni mwa mwaka huu.

“Mwaka jana tulitoa washindi 19 na tunaahidi kubadili maisha kwa Watanzania kupitia michezo yetu mbalimbali ya kubahatisha,” alisema Mushi.

Alisema kuwa wameongeza odds (alama za ushindi) kwa wateja wao wa kubeti ili kuwawezesha kupata fedha nyingi zaidi.

Kwa upande wake, Ngolo alisema kuwa hakuamini kama ameshinda kiasi kikubwa cha fedha pamoja na kupewa taarifa na Mushi wa M-Bet.

“Mimi ni fundi matreta, nilikwenda kufanya kazi eneo ambalo halina mtandao wa simu, wakati nikiwa njiani narejea kazini, nikapokea simu kutoka kwa Mushi, sikuamini mpaka nilipo hakikisha kwenye mkeka wangu,

Kitu cha kwanza ni kutumia fedha hizi kufungua karakana na duka la vipuri (spea), hapa nitakuwa nimezuia kutoa fedha kununua maduka mengine, mambo mengine ya maendeleo yatafuata,” alisema Ngolo.

Alisema kuwa ushindi wake ni matunda ya kutokata tamaa kwani alianza kubashiriki mwaka 2015 na kiasi kikubwa cha fedha alizoshinda ilikuwa Sh 1.8 milioni.
Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa droo ya kwanza ya mchezo wa kubaatisha ya Perfect 12, Mohamed Ngolo aliyejishindia Sh milioni 166. 3.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...