Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni ya uhamasishaji ikilenga kuwashawishi zaidi wateja wa benki hiyo kutumia kadi za MasterCard ambapo pamoja na mambo mengine itatoa zawadi mbalimbali kwa wateja hao.

Uzinduzi wa kampeni hiyo mpya iliyopewa jina la 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' unalenga kutoa fursa ya kipekee kwa wateja wa benki hiyo kufurahia huduma zinazokwenda sambamba na mfumo wa maisha yao kupitia benki hiyo.

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Andrew Lyimo, kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi za benki hiyo katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.

"Kwa upande wetu Benki ya Exim, wateja wanaotumia kadi zetu wamekuwa wakifurahia urahisi wanapofanya manunuzi au malipo kwenye ya mahitaji muhimu kwenye maduka (Shopping), ununuzi wa bidhaa kimataifa kupitia mtandaoni, malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli na shughuli za kitalii. '' Alisema.

"Na kwa sasa, si tu kwamba wateja wetu wanafurahia urahisi mkubwa unaotokana na matumizi ya kadi za benki ya Exim, bali pia wanapata fursa ya kushinda zawadi nzuri kupitia kampeni hii. Kutakuwa na zawadi za kila wiki, kila mwezi na kubwa za mwisho wa kampeni. Wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya miamala yao kupitia kadi ya Exim Bank MasterCard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kila muamala unaongeza nafasi moja ya kushinda,'' aliongeza.

Alibainisha kuwa wakati wa kampeni hiyo, jumla ya washindi 10 wa kila wiki watapata zawadi za vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi 50,000 huku kila mwezi washindi watano (5) watazawadiwa simu janja (smartphones).

Akizungumzia zawadi kubwa kwenye kampeni hiyo Bw Lyimo alisema washindi pamoja na wenza wao watatunukiwa zawadi ya kusafiri wakiwa wamegharamiwa gharama zote ikiwemo Visa, Tiketi ya Ndege pamoja na pesa za matumizi.

"Mshindi wa kwanza ataenda Dubai, mshindi wa pili ataenda Cape Town, Afrika Kusini na wa tatu ataenda visiwa vya Zanzibar.'' alitaja.

Kwa mujibu wa Bw. Lyimo, Kampeni hiyo imeanza katikati ya mwezi Februari hadi mwisho wa mwezi Aprili 2020 na ipo wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi za Exim Bank MasterCard, pamoja na wateja wote ambao wameomba au wataomba kadi mpya katika kipindi cha kampeni.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bwana Stanley Kafu, alielezea kufurahishwa kwake na uzinduzi wa kampeni hiyo akisema, "Tumefurahishwa sana na ujio wa kampeni ya Chanja Kijanja. Kuongeza ubora wa huduma za kibenki kwa wateja wetu huku tukifanya matumizi yao kuwa na faida kwao, ndio falsafa ya kiutendaji hapa benki ya Exim'' alisema.

"Benki ya Exim itaendelea kutoa ofa na zawadi za kipekee kwa wateja wake, kama ishara ya kuthamini imani na uaminifu wao kwetu. Ni furaha kwetu kuona tunagusa hisia za wateja wetu kupitia kampeni hii. Kutumia kadi ya Exim Bank MasterCard ni njia ya haraka, rahisi na salama ya kufanya ununuzi wa kila siku…hivyo basi wewe Chanja Kijanja na Exim Bank Mastercard,'' alisisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...