Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii 

SHIRIKA la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) likamilisha mtaala mpya wa kilimo ambao unatarajiwa kuanza kutumia kwenye vyuo vya mafunzo ya kilimo 29 nchini ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha mtaala huo unaendana na mahitaji ya sasa. 

Akizungumza na waandishi wa habari za kilimohai wakati wa mafunzo maalumu ya kilimo hicho, Meneja wa Mradi wa SAT Mgeta Daud amesema mtaala huo wameufanikisha kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Divisheni ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti kwa hisani ya Shirika la Maendeleo la Leichtenstein. 

Amefafanua awamu ya kwanza ya mtaala huo ulianza kufundishwa katika vyuo saba vya Mati Kartini, Chuo cha Taifa cha Sukari(NSI), Mati-Ilonga, Mati horti-Tengeru, KATC-Moshi, TRACDI na Chuo cha St.John's. 

"Mradi huu unaendelea kupanua wigo wake na kufikia vyote vyote 29 vya mafunzo ya kilimo nchini katika kanda zote saba za kilimo.Mradi huu ambao unafahamika kama CISTI unatekelezwa katika ngazi tatu kuu.Ngazi ya kwanza mradi unajenga uwezo wa wakufunzi wa vyuo vilivyopo katika mradi. 

"Katika ngazi ya pili mradi unaimarisha uwezo wa vyuo ya mafunzo ya kilimo kimiundombinu ili kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa mtaala mpya wa kilimo na tatu mradi unashirikiana na divisheni ya mafunzo, huduma za ugani na utafiti ya wizara ya kilimo ambayo ndiyo ina dhamana ya kusimamia vyuo vyote vya kilimo kuhakikisha mtaala unatekelezwa vyema na matokeo chanya yanatokea,"amesema Daud. 

Akifafanua zaidi kuhusu mtaala huo,amesema matokeo ya upembuzi yakinifu wa hali halisi ya soko la ajira , hali halisi ya vyuo vya mafunzo ya kilimo na uwezo wa wakufunzi katika kufundisha mtaala, ulisababisha kuanza mchakato wa kuhuisha mtaala uliokuwepo ili uendane na mahitaji ya sasa ya maarifa na utalaamu unaohitajika katika soko la ajira. 

Ameongeza Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania lilishiriki kikamilifu katika hatua zote za muhimu za kuhuisha mtaala na hatimaye ushawishi wake ulisababisha kuingizwa kuingizwa kwa moduli mpya tatu za kilimo hai, jinsia katika kilimo na usimamizi wa mazingira katika mtaala mpya. 

"Mchakato wa kuihusha mtaala ulikamilika baada ya taratibu zote kufuatwa na kuthibitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa(NACTE)na kilele cha mchakato huu kilihitimishwa kwa kuzinduliwa kwa mtaala mpya ambao ndio unachukua nafasi ya mtaala wa zamani,"amesema. 

Mbali ya kuzungumzia mtaala huo mpya, ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa SAT pamoja na mambo mengine ya kilimo ikiwemo ya kufanya tafiti, yenyewe imejikita katika kilimohai ambacho kinalenga katika kuleta uendelevu wa rutuba ya udongo, bioanuai, na hifadhi ya mazingira huku afya za walaji wa vyakula vya kilimo hicho zikilindwa na kuboreshwa. 

"Kuna taasisi na kampuni takribani 30 yanajihusisha na kilimo hai na wakulima wapatao 148,610 na eneo la hekta 268,729 nchini Tanzania.Namna bora ya kuongeza wigo wa kilimo hai Tanzania ni kuzalisha wageni wenye umahili katika maarifa na ujuzi wa kilimo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro akionesha zao la bizali ambalo linalimwa katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo hai ambacho kinamilikiwa na Shirika hilo
:Mmoja ya waandishi wa habari kutoka Capital TV ambaye pia ni Mshauri wa masuala mbalimbali katika jamii Austine Makani akifuatilia kwa makini maelezo ya watalaamu wa kilimo hai katika Kituo cha Utafiti cha kilimo kinachomilikiwa na Shirika la kilimo Endelevu (SAT).
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika moja ya bwawa la kufugia samaki baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT).
Mkurugenzi Mtandaji wa SAT Janeth Maro akiwa ameshika jani la Mnyonyo wakati anaeleza faida ya jani hilo katika kukomesha wadudu waharibifu wa mazao.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya kilimo hai yaliyofanyika katika Kituo cha Utafiti wa kilimo kinachomilikiwa na SAT.
Mkurugenzi Mtandaji wa SAT Janeth Maro akiwa ameshika jani la Mnyonyo wakati anaeleza faida ya jani hilo katika kukomesha wadudu waharibifu wa mazao.





Mbogamboga za majani zikiwa zimepandwa katika mfuko maarufu kwa jina la kiroba .Mfumo huo wa upandaji wa mbogamboga unatumia eneo dogo.
Meneja wa Mradi wa Mtaala mpya wa kilimo kutoka Shirika la Kilimo Endelevu( SAT) Mgeta Daud akizungumzia kukamilika kwa mtaala huo ambao unatarajiwa kuanza kutumia kwenye vyuo 29 nchini na kwamba mtaala huo umekamilika kwa ushirikiano kati yao na Wizara ya Kilimo kupitia Divisheni ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti kwa hisani ya Shirika la Maendeleo la Leichtenstein.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) Janeth Maro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo zimetumika hadi kukamilika kwa mtaala huo wa ambao utakwenda kutumika kwenye vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo nchini kwa ngazi ya cheti na Diploma.
Mazao mbalimbali yakiwemo kweye 'Green House' katika eneo la Kituo cha Utafiti cha kilimo Hai ambacho kinamilikiwa Shirika la Kilimo Endelevu( SAT).Kituo hicho kimekuwa kikitumika kutoa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali yakiwemo ya kufanya tafiti mbalimbali za kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...