Baadhi ya wakulima wa kilimo hai mkoani Morogoro wakiwa katika moja ya mkutano wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kilimo hicho ambapo wametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Serikali kuanzisha bodi ambayo itahusika kusimamia mazao ya kilimo hai yakiwemo mazao ya viungo ambayo yamekuwa yakilimwa na baadhi ya wakulima ambao wako chini ya mradi wa unaosimamiwa na Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT).
Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu kilimo cha viungo ambacho kinalimwa na baadhi ya wakulima katika wilaya ya Morogoro Vijijini na Mvomero mkoani Morogoro
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAT (hayupo pichani) wakati akielezea jitihada ambazo zinafanywa na shirika lake katika kutafuta masoko ya mazao ya viungo ndani na nje ya Tanzania.
Janeth Maro ambaye ni Mkurugezi Mtendaji wa SAT akisisitiza jambo kuhusu kilimo cha viungo



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

WAKULIMA wa mazao ya viungo mbalimbali vinavyotokana na kilimo hai mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuunda bodi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia bidhaa zao kama ilivyokuwa kwenye zao la pamba ili kuhakikisha wananufaika na kilimo hicho.

Wametoa ombi hilo baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti cha Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania kilichopo mkoani Morogoro ambapo wakulima hao wanatoka katika Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Lubondo.

Wakulima hao wamesema pamoja na kupatiwa mafunzo ya kilimo hai na wao kujikita katika kilimo cha viungo mchanganyiko lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni soko la uhakika.

Mmoja wa wakulima na mfugaji kutoka katika kijiji hicho cha Lubondo Pendo Ndeme amesema wanatoa shukrani kwa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) kwa kuendeleza kilimo hai mkoani hapo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ya kutoa elimu ya kilimo hicho na namna ya kukiendleza.

Amesema SAT Imekuwa na mchango mkubwa hasa katika kutoa elimu ya kilimo hai, hivyo wao kama wananchi ambao wanatoka katika kata ya Lubondo ,kijiji cha Lubondo wameweza kuhamasika na kujikita katika kilimo cha viungo mbalimbali na kwa kiasi kikubwa wanafanya vizuri lakini changamoto kubwa wanayoipata ni soko la uhakika.

Ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Serikali kuangalia upya katika eneo hilo kwani kama watawawezesha kwa kuwapatia bodi ya yao kuwasimamia kama ilivyo kwenye zao la pamba wanaamini watanufaika zaidi na kilimo hicho cha viungo ambacho kwa sasa wanaona faida yake.

"Hivi sasa tunazalisha kwa wingi mazao ya viungo lakini tatizo kubwa ni soko pamoja kwamba shirika la SAT linajitahidi kutafuta masoko kwa ajili wakulima bado tunaona iko haja kwa Serikali kuongeza nguvu katika eneo hili, SAT wametuhamasisha kulima na wakulima tumeitikia kwa mwitikio mkubwa sana,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro amesema wanatambua faida za kilimo cha mazao ya viungo na kupitia miradi mbalimbali ambayo wamekuwa wakifanya kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho kimetoa hamasa kwa wakulima wa mkoa huo na hasa wa Wilaya ya Mvomero na Morogoro Vijijini.

‘’SAT pamoja na mambo mengine yanayohusu kilimo hai tumekuwa na jukumu la kuhakikisha tunatafuta soko kwa ajili ya kuhakikisha mazao ya wakulima ambayo yanazalishwa yanapata soko la uhakika na ndio maana baadhi ya mazao tumeyayatafutia soko nchi za nje ikiwemo nchi ya Uswis,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...