Mary-Salome Masoi
22 Oktoba 1939 – 24 Januari 2020
Familia ya Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Willy John Masoi ya Ukonga Saba Saba jijini Dar es salaam, inapenda kutoa shukrani za dhati kufuatia misaada mbalimbali iliyotolewa kufuatia kifo cha Mama yetu mpendwa Mary-Salome Masoi kilichotokea tarehe 24 Januari 2020 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam hadi mazishi tarehe 30 Januari 2020 Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Misaada ya hali na mali pamoja na faraja kutoka kwenu vilikuwa na vimeendelea kuwa na mchango mkubwa katika maisha yetu sasa na hata baadaye. Shukrani za pekee ziwaendeee madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Mapadri walioongoza Ibada ya Mazishi ya Mama yetu Mpendwa wakiongozwa na Padri Stephen Nyilawila (Parokia ya Mt. Augustino - Ukonga), Padri John Mallya (Epiphania - Mtoni Kijichi), Padri Paul D. Malewa (BMMK - Bunju), Padri Dyfrig J. Maliti (Shirika la Roho Mtakatifu-CSSP), Padri Stefano Kaombe (Mt. Francis Ksavery -Chang’ombe), wanajumuiya ya Mt. Monika wa Parokia ya Mt. Augustino - Ukonga, Taasisi mbali mbali za Kiserikali, Kimataifa na Binafsi, vikundi vya kidini na vya kijamii, bila kusahau majirani, ndugu, jamaa, na marafiki walioshiriki pamoja nasi tangu Mama yetu alipolazwa hospitalini tarehe 11 Januari 2020 hadi tulipompumzisha katika nyumba yake ya milele. Sisi wanafamilia, tunasema “ASANTENI SANA! MWENYEZI MUNGU AWABARIKI”.
"Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki.” 2TIMOTEO 4:7
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...