Na.Khadija seif, Michuzi Tv
MSANII
wa singeli Mwarami Sadick maarufu Kama meja kunta alietamba na kibao
cha ooh mamuu amepata ajali alfajiri ya kuamkia leo maeneo ya segera
mkoani Tanga.
Akizungumza na Michuzi Tv kupitia simu Meneja wa Meja Waso wiso amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Tumepata
ajali maeneo ya segera Tanga na kwenye gari tulikua na cameraman,dj
,mimi pamoja na Meja mwenyewe tumegongana na gari ambapo ajali inatokea
meja alikua amelala na yeye ndio ameumia sana,"
Hata
hivyo waso wiso amesema ilikua ngumu kwao kupata msaada wa haraka
kutokana na ilikua asubuhi sana na kumtaja madee pamoja na Naibu waziri
wa maji Juma Aweso kuwa msaada kwao.
"Madee
alikua ni miongoni mwa wasanii ambao walikua wanaelekea kwenye Tamasha
la Muziki mnene hivyo ikawa rahisi kutuona barabarani akisaidiana na
Naibu waziri wa maji Juma Aweso na kutupatia msaada wa haraka.
Hata
hivyo Waso ameeleza kuwa Hali ya Meja sio nzuri hivyo wamelazimika
kumkimbiza hospitali ya mkoa ili kupatiwa matibabu zaidi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...