Charles James, Michuzi TV

WAMEKIMBIA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lundo la madiwani 11 wa Jiji la Mbeya wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao 11 wakiongozwa na Meya wa Jiji hilo, David Mwashilindi na Katibu wa Wilaya wa Chadema wametangaza kuhamia CCM leo jijini Dodoma na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk Bashiru Ally.

Akizungumza baada ya kuwapokea kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dk Bashiru amesema wingi huo wa madiwani umevunja rekodi na kwamba sasa wapinzani wamekwisha Mbeya.

Madiwani hao ambao kata wanazoongoza  ziko kwenye mabano ni Fabian
Sanga (Ghana), Fanuel Kyanula (Sinde) ambaye pia ni Naibu Meya,
Davidi Mwashilindi (Nzouwa) ambaye ni Meya, Anyandwile Mwaluhubh
(Isanga), Kigenda Kasebwa (Ilomba Viti Maalum) na Dickson Mwakilasa
(Ilomba).

Wengine ni Costantine Mwakyoma (kalobe) Furaha Mwandalim (Ilemi) Henry Mwangambaku (Forest) ambaye pia ni katibu wa Wilaya, Anderson Ngao (Mwasanga) na Ibrahim Mwampwani (Isyesye).

Jiji la Mbeya linaongozwa na Mbunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambalo limekua likitajwa kama mojawapo ya ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani lakini kuhama kwa madiwani hao 11 kumetoa mwanya kwa CCM kuanza kuwa na matumaini makubwa kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

" Hii si mara ya kwanza kupokea madiwani na meya kwa wakati mmoja tulishapokea meya wa Ilala, meya wa Jiji la Arusha na huu ni
muendelezo tu.

Niwahakikishie ujio wa madiwani hawa ni uthibitisho tosha wa namna gani Rais Dk John Magufuli na serikali yetu ya CCM inafanya kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi kiasi cha viongozi wa upinzani kuamua kwa mapenzi yao kuunga mkono," Dk Bashiru.

Aidha Dk Bashiru amekanusha taarifa zinazosambwa mitandaoni zikionesha gari la Katibu Mkuu wa CCM likilindwa na Jeshi la Polisi ambapo amesema ni uongo na zile picha zinazosambazwa ni za kutengeneza.

Akizungumza baada ya kupokelewa na Dk Bashiru, Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi amesema yeye sio Chadema tena na amerudi kwenye chama chake kilichomlea na ambacho kimekua kikishughulika na kero za wananachi.

" Ndugu zangu sijataka kuwa mnafiki, kwa miaka minne ya Rais Magufuli nimeshuhudia kazi kubwa ambayo kwa hakika imekua sababu tosha ya mimi kurejea CCM, Rais aliahidi na anatekeza.

Chini ya Magufuli kila sekta imeguswa, afya, miundombinu, elimu na zaidi mafisadi hawapo awamu hii, kuendelea kubaki upinzani ni kukosa uzalendo, Chadema kule hakuna ajenda zaidi ya ugomvi na kupinga mambo makubwa yanayofanywa," Amesema Mwashilindi.
 Meya wa Jiji la Dodoma anayetokana na Chadema ambaye amehamia CCM, David Mwashilindi akizungumza baada ya kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk Bashiru Ally jijini Dodoma leo.
 Wandishi kutoka vyombo mbali mbalimbali na madiwani wa Chadema waliohamia CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM , Dk Bashiru Ally jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk Bashiru Ally akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma baada ya kuwapokea madiwani 11 wa Jiji la Mbeya wanaotokana na Chadema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...