Charles James, Michuzi TV

SERIKALI za Tanzania na Finland zimekubaliana kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii nchini pamoja na sekta zingine za kimaendeleo lengo likiwa ni kuinua uchumi wa Nchi.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara, Ville Skinnari.

Akizungumza baada ya mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Finland nchini, Riita Swan, Katibu Mkuu Prof Mkenda amesema serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje ya Nchi kuja kuwekeza na kufanya biashara.

Amesema katika mazungumzo hayo yalijikita katika kuzungumzia manufaa ya misitu na namna ambavyo wataweza kumaliza changamoto ya uchomaji misitu na kuhamasisha upandaji miti.

" Tunawashukuru wenzetu wa Finland ambao kwa hakika tumekua tukishirikiana kwa muda mrefu, tumejadili kwa pamoja umuhimu wa kuendeleza nishati mbadala ili kuepuka matumizi ya mkaa ambayo husabahisha uchomaji wa misitu.

Lakini wao pia wametuahidi kutusaidia katika uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu kwani wao wamekua ni wabobezi kwenye eneo hilo," Amesema Prof Mkenda.

Amesema pia wamewaalika wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza kwenye viwanda hivyo ikiwa ni sera ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

" Tumemualika Mhe Waziri kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu ili awe Balozi mzuri wa kututangaza na kuhakikisha tunanufaika na wingi wa watalii wanaotoka Finland.

Pia tumewaalika kuja kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini kwetu hasa katika eneo la Hoteli na tumewahakikishia kwamba mazingira ni salama na tutawapa ushirikiano wote," Amesema Prof Mkenda.

Kwa upande wake Waziri huyo wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara, Mhe Ville Skinnari amesema wamekuja Tanzania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wizara mbalimbali ili kuendeleza ushirikiano wa Nchi hizi mbili pamoja na kufungua Milango ya uwekezaji.

Amesema sekta ya utalii imekua ikifanya vizuri na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna ambavyo serikali yake imetengeneza sera nzuri zinazovutia watalii na wawekezaji kwa ujumla.

" Tumewaeleza wenzetu kwamba suala la utunzaji wa mazingira hasa kulinda misitu yetu ni muhimu sana, tumewaahidi tutashirikiana katika kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu ili kuongeza pia fursa ya ajira na kukuza uchumi wa Nchi," Amesema Skinnari.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kikao chake na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Ville Skinnari (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kikao chake na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii (kulia) leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Ville Skinnari akimkabidhi zawadi ya Tai Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda baada ya kumalizika kwa kikao chao leo jijini Dodoma.
 Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii (kulia) wakiwa kwenye kikao cha pamoja na viongozi kutoka serikali ya Finland. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...