
Ligi Kuu ya Vodacom:
Mechi
namba 150: Simba SC 3 v Namungo FC 2-Mwamuzi msaidizi namba mbili
Kassim Safisha amefungiwa miaka mitatu(3) kwa kosa la kushindwa
kutafsiri sheria ya kuotea katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 29,2020
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa
mujibu wa Kanuni namba 39(1)(a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Mechi
namba 157: Azam FC 1 v Mtibwa FC 1-Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa
barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika
mechi iliyochezwa Januari 30,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Vile vile katika
mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya
Makamishina kwa kosa la kutoa taarifa yenye mapungufu.Adhabu hii ni kwa
kuzingatia Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina
Ligi Daraja la Kwanza:
Mechi
namba 75A :Friend Rangers(0) vs Dodoma FC(1)-Kiongozi wa Klabu ya
Friends Rangers Heri Chibakasa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kupigana na
washabiki wa timu pinzani
Ligi Daraja la Pili:
Mechi
namba 29A:Dar City Fc (1) vs African Sports(0)- Mwamuzi Salum Mkole
amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kuonyesha udhaifu katika usahihi wa
kutoa kadi katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 31,2020 katika uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni
namba 39(1) kuhusu Udhibiti wa Waamuzi katika mechi iliyochezwa
Februari 01,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Vile
vile katika mchezo huo mchezaji wa Klabu Ya African Sports Rajabu
Kipango amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Timu pinzani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...