Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa na Mkurugenzi wa PRNG Lucas Stanfield kulia ofisini kwake jijini Dodoma.
*****************************
Na Issa Mtuwa – Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amesema utaratibu wa upatikanaji wa leseni za madini za aina mbalimbali hupatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Amesema, sheria hizo hutumika kulinda leseni hizo ili ziwe hai. Kwa kuzingatia masherti yaliyomo kwenye leseni, atakayeshindwa kuzingatia masherti hayo sheria hutumika ikiwemo kutoa hati ya makosa (default notes) na hatimae kuzifuta.
Biteko ameyasema hayo leo tarehe 6/02/2020 wakati wa kikao chake na kampuni ya Peak Resources Ngwala (PRNG) ofisini kwake jijini Dodoma akizungumzia masuala ya utoaji wa leseni za uchimbaji madini. PRNG walikuwa wakifuatilia upatikanaji wa leseni ya uchimbaji madini ambapo Biteko amesema suala lao linashugulikiwa na taratibu zikikamilika
watapatiwa.
Amesema wakati wa sasa suala la leseni siyo kificho na halihitaji kumuona mtu ili upate leseni, kubwa ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuzingatia sheria. Ameongeza kuwa leseni ya PRNG ikikamilika itatolewa.Mkurugenzi wa PRNG Luca Stanfield amemshukuru waziri kwa mazungumzo yake huku wakisema wanachosubiri kupata leseni ili waanze kazi na watafwata sheria.
Biteko amesema leseni zinatolewa kwa kila mtu iwe wa ndani au nje ya nchi anapaswa kuzingatia sheria na taratibu. “Kwenye utoaji wa leseni kuna sheria za kuzingatia ikiwemo ulipaji tozo za kodi za serikali ambazomuombaji anapaswa kuzifahamu na kulipa” amesema Biteko.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...