Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) wamesherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama.

Sherehe hizo hufanyika  ifikapo Februari 22 kila mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam  Kamishina mkuu wa TGGA Tanzania Symphorosa Hangi amesema wameweza kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kufanya shughuli za kijamii katika maeneo tofauti nchini pamoja na kuchangia damu.

Amesema, wamefanya shughuli za kijamii wiki moja kabla wakishirikiana na jamii inayowazunguka ili kudumisha upendo na furaha waliyoachiwa na waasisi wao.

Hangi amesema, wamehitimisha siku hiyo muhimu kwa kuchangia damu salama ili kuwasaidia wamama wajawazito na wanaopata ajali.

Amesema, wanaishukuru hospitali ya Muhimbili kwa kushirikiana nao ambapo wameweza kupeleka watoa huduma wa kutosha sambamba na wananchi waliojitokeza kuchangia damu kama kudhihirisha upendo kwa wale wahitaji waliopo mahospitalini.
 Kamishina mkuu wa wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) Tanzania Symphorosa Hangi akizingumza na wafanyakazi wa Chama hicho, wageni waalikwa pamoja na wanafunzi ambao ni Girl Guides wakati wa kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama katika ofisi zao zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
 Katibu taifa wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA),Bupe Minga akizungumza jambo wakati wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni na kushiriki katika kuchangia damu salama leo jijini Dar es Salaam.

 Muuguzi kutoka Kitengo cha Damu  upande wa utoaji Damu Muhimbili  Angelina Madeni(kulia)akipima ujazo wa damu aliyokuwa anaitoa Rafiki wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mwisho Mwampamba(kushoto)  wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni.
Labaratory  Scientistic kutoka Muhimbili Amos Nzile akiweka mpira wa kutoa damu kwa Mwalimu wa Diamond Primary school Agnetha Manjoli  wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni.
Mratibu wa mradi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Valentina Gonza akipimwa damu na Mtekinologia wa Maabara kutoka katika hospitali ya Muhimbili, Makanga Leonard kwa ajili ya kutoa damu wakati wa wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni na kushiriki katika kuchangia damu salama leo jijini Dar es Salaam.
 Labaratory  Scientistic kutoka Muhimbili Amos Nzile  akiangalia mshipa utakaoweza kutoa damu kwa Rafiki wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Tuli Minga wakati wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama katika ofisi zao zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Katibu taifa wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA),Bupe Minga(kushoto) akijaza fomu kwa ajili kuchangia damu wakati wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama katika ofisi zao zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mfanyakati wa Benki ya Damu kutoka muhimbili Joash Michael.

 Zoezi la uchangiaji wa damu likiendelea wakati wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama katika ofisi zao zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi na waanzilishi wa Girl Guides Ulimwenguni kwa kuchangia damu salama katika ofisi zao zilizopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...