*Vibali na Usajili vilihusisha  Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanshi
*Yapiga hatua katika uanzishaji wa viwanda vya dawa,vifaa tiba Kanda ya Ziwa.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii ,Mwanza

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imesajili  na kutoa vibali  vya majengo ya biashara  ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitandanishi  2,043.

Usajili  na utoaji wa vibali ilitokana na TMDA Kanda ya ziwa  baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha  kuwa majengo yankidhi vigezo vya utunzaji wa ,usambazaji ,uuzaji na utengenezaji wa bidha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari  na Timu ya Maafisa wa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto , Meneja wa Kanda ya Ziwa  Sophia Mziray  amesema kuwa  katika Miaka minne ya Utawala wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli wamefanikiwa kutokana na serikali kuwekeza maabara ya uchunguzi wa dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa za afya zilizo bora.

Amesema kuwa TMDA  kwa kanda Ziwa imetoa ushauri wa kitaalamu katika kiwanda cha dawa  kimoja cha jijini Mwanza pamoja na ushauri wa wa kiufundi kwa kwa viwanda saba  vipya vya tiba  na viwanda vinne vya vipya vya dawa za maji na sindano.

Mziray amesesma  TMDA imeweka wakaguzi katika mipaka  vituo vya forodha vya Sirari, Mtukula na Bandari ya Mwanza Kusini ambao ndio wakaguzi wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kuruhusu kuingia au kutoka nje ya nchi mara tu baada ya kujiridhisha katika ukaguzi.

Aidha amesema kuwa wameanzisha mfumo  wa Kieletroniki wa uombaji wa vibali na utoaji kwa masaa 24 ambapo kupitia mfumo huu mkaguzi aliyeko mpakani ay bandarini anaweza kuhakikisha kibali kilichotolewa na mamlaka wakati wa kufanya ukaguzi wa bidhaa inayoingia kutoka nje ya nchi hadi sasa jumla ya vibali 2552 vimetolewa.

“Kwa kazi inayofanyika inaonyesha kuwa elimu ya udhibiti kwa wadau wetu imeeleweka  na hivyo kukidhi matakwa ya kisheria ya uingizaji na utoaji wa bidhaa nje ya nchi”amesema Mziray.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya Tano Shehena/Mizigo 6,668 vya dawa ,Vifaa Tiba na Vitendanishi vilikaguliwa katika vituo vya forodha 10 ambavyo ni Sirari,Mtukula,Rusumo,Mulongo, Kabanga, Bandari ya Kusini  Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Mwanza,Bandari ya Ziwa  Musoma,  Bandari Kavu ya Isaka  na  Bandari ya Kamondo  Bay na mizigo ambayo   haiikukidhi vigezo vya ubora na usalama ilizuiliwa na baadae kuteketezwa na zingine bidhaa zilirudishwa katika nchi zinakotoka.

 Afisa Mwandamizi wa Ukaguzi  wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bugaru Nyamweru akionesha maabara za uchunguzi ambazo serikali imewekeza kwa shi.bilioni Saba wakati wanadishi na maafisa habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na Watoto walipotembele TMDA Kanda ya Ziwa,
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Sophia Mziray akizungumza na waandishi habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto , Meneja wa Kanda ya Ziwa  Sophia Mziray  amesema kuwa  katika Miaka minne ya Utawala wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli wamefanikiwa kutokana na serikali kuwekeza maabara ya uchunguzi wa dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi katika kanda hiyo.
 Picha ya Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Sophia Mziray pamoja Waandishi Habari , Timu ya Maafisa wa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto  walipotembelea  TMDA Kanda ya Ziwa.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...