Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, wakiwa wamemmbeba mwenzao, kama mfano wa kumpa huduma ya
kwanza mtu aliyepata ajali ya kuvunjika viungo, kwenye zoezi la upimaji
wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi,
yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma
Februari 1, 2020.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, wakimsikiliza Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza (OSHA), Moteswa
Meda, wakati akiwaelekeza mfano wa kumpa mtu huduma ya kwanza pindi
anapopata dharura, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA
kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya
Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020.
Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Thomas Salila, akipimwa usikivu wa masikio na Mkaguzi wa Afya MAMLAKA ya
Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Zakayo Mmbaga, kwenye zoezi la
upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi,
yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma
Februari 1, 2020.
Kaimu Mtendaji Mkuu, MAMLAKA ya
Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda, ukitoa elimu
kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, kwenye zoezi la upimaji wa afya na
mafunzo ya OSHA , yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa,
jijini Dodoma Februari 1, 2020.
Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Fredrica Shirima, akipimwa urefu na Mkaguzi wa Afya MAMLAKA ya Usalama
na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Saredho Hussein, kwenye zoezi la upimaji
wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi,
yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma
Februari 1, 2020.

Katibu wa Waziri Mkuu Bw. Raymond
Gowelle, akikabidhiwa cheti cha ukaguzi katika maeneo yote ya ofisi hiyo
na Kaimu Mtendaji Mkuu MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi
(OSHA), Khadija Mwenda, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya
OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya
Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………………………..
MAMLAKA ya
Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imetoa cheti kwa Ofisi ya Binafsi
ya Waziri Mkuu baada ya kufanyia ukaguzi katika maeneo yote ya ofisi
hiyo na kuonesha kuwa yamekidhi viwango.
Cheti hicho
kimetolewa jana jioni (Jumamosi, Februari 1, 2020) na Kaimu Mtendaji
Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda na kupokelewa na Katibu wa Waziri Mkuu
Bw. Raymond Gowelle.
Akikabidhi
cheti hicho, Bi Khadija aliipongeza Ofisi hiyo kwa kuonesha mfano wa
uetekelezaji wa sheria, ambapo amezishauri ofisi nyingine za umma ziige.
“Ofisi
Binafsi ya Waziri Mkuu imeonesha mfano wa kuigwa kwa utekelezaji wa
sheria, kwani walituita tukaja kufanya ukaguzi na tukatoa maelekezo ya
namna ya kuboresha baadhi ya maeneo na wamerekebisha.”
Alisema baada
ya kutekeleza maelekezo hayo suala lililokuwa limebakia ni upimaji wa
afya kwa wafanyakazi pamoja na kutoa mafunzo ya huduma ya kwanza ambayo
yamefanyika leo (jana).
Mtendaji huo
alisema ni muhimu kwa ofisi zote kuzingatia sheria ya Usalama na Afya
Mahali pa Kazi kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Baada ya
kukamilisha zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA, pia watumishi
wa Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu walikumbushwa namna bora ya kufanyakazi
kwa uadilifu. Mafunzo yalitolewa na watalaamu kutoka Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Watumishi hao
waliushukuru uongozi wa ofisi kwa kuandaa zoezi la upimaji wa afya
ambao ulikuwa na muitikio mkubwa, mafunzo ya huduma ya kwanza pamoja na
kukumbushwa kuhusu uadilifu na matumizi ya madaraka na ofisi kwa manufaa
ya umma.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...