Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), imeshauriwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa kwa
kuwa Tanzania ni nchi mojawapo za ukanda wa Afrika Mashariki yenye lango kuu la
kuingilia ukanda huo suala linalosaidia kukuza uchumi kupitia ushuru wa forodha
unaotozwa katika eneo hilo.
Ushauri huo umetolewa jana
na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya alipotembelea
TRA akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini
"Ili kusimamia ushuru
wa forodha ipasavyo, suala la teknolojia halikwepeki, hivyo ni muhimu TRA
ijikite zaidi katika kuendelea kuwekeza kwenye mifumo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuwa na watumishi wenye uwezo wa kuendesha mifumo hiyo",alieleza.
Dkt. Kunio Mikuriya alisema
kwamba, akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede, wamezungumzia juu ya umuhimu wa
matumizi ya teknolojia katika kudhibiti na kusimamia ushuru wa forodha kwenye
bandari ya Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naye, Kamishna Mkuu wa
TRA alisema kuwa, ziara ya Katibu Mkuu huyo imelenga kuimarisha mahusiano baina
ya nchi wanachama wa WCO ambapo ametokea nchini Kenya kwa ajili ya kazi hiyo
pia.
"Tanzania ni mwanachama
wa WCO na kuna mashirikianio ambayo tunafanya kwa pamoja kuhakikisha eneo la
forodha linatekeleza majukumu yake ili kuhakikisha kuna usalama wa bidhaa kwenye
eneo la biashara",alisema Dkt. Mhede.
Alisema kuwa, Tanzania
ni kitovu cha biashara kwa kuwa inahudumia nchi zote ambazo hazina bandari kwa
mfano Zambia, Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao wote wanatumia
Bandari ya Dar es Salaam, hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika
kusimamia masuala yote ya kiforodha.
Katibu Mkuu wa WCO
Dkt. Kunio Mikuriya baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania alielekea
jijini Dodoma kwa lengo la kukutana na baadhi ya watunga sera kwa ajili ya
kuimarisha mahusiano yaliyopo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akimpa zawadi
ya jarida linaloonesha vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini Katibu Mkuu wa Shirika
la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya wakati alipotembelea
TRA jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede wakipeana mikono mara baada ya Kamishna Mkuu kumkabidhi zawadi Katibu Mkuu huyo ambaye alitembelea TRA jana jijini Dar es Salaam ili kuona shughuli mbalimbali hususani za kiforodha zinazofanywa na TRA.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya (kushoto) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea TRA jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea TRA jana jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akiwa na mgeni wake Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO) Dkt. Kunio Mikuriya (wa pili kulia) wakielekea eneo la forodha la Bandari ya Dar es Salaam wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea TRA jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Msaidizi wa TRA Joseph Raymond akimuonesha Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO) Dkt. Kunio Mikuriya mfumo mpya wa kukagua mizigo inayoingia na kutoka nchini wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea TRA jana jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...