Na Khadija Khamis
– Maelezo Zanzibar 06/07/2020.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mohamoud
Thabit Kombo amewataka wahariri wa
vyombo vya habari nchini kuitumia lugha ya Kiswahili fasaha kwa lengo la
kufahamika na jamii
Hayo aliyasema
huko katika Ukumbi wa Wizara ya habari utalii na mambo ya kale Kikwajuni wakati
wa Mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya
Habari vya Zanzibar .
Alisema utumiaji
wa lugha ya Kiswahili fasaha utasaidia
muongozo mzuri wa kufahamika na jamii pamoja na kuilinda lugha ya Kiswahili
isipotee.
Aidha alisema
Wahariri, Waandishi wa Habari pamoja na Watangazaji ni vyema kuisimamia lugha hiyo ili iweze
kurekebisha mapungufu yanayojitokeza katika matamshi .
Alifahamisha
kuwa katika kuikuza lugha ya Kiswahili sanifu ili itumike kama inavyohitajika Baraza
la Kiswahili (BAKIZA) wameweza kusambaza makamusi katika vituo vya Habari
nchini.
Waziri huyo
alisema baada ya mafunzo hayo anatarajia mabadiliko makubwa katika utumiaji wa lugha
ya Kiswahili fasaha kwa Watangazaji wa Vyombo vya Habari ikiwemo Radio Televisheni pamoja na Magazeti
Nae Katibu Mtendaji
wa Baraza la Kiswahili (BAKIZA) Dkt Mwanahija Ali Juma alisema tafiti mbali
mbali zimeshafanywa na baraza hilo na kuweza kuona makosa ya Kiswahili sanifu yaliyofanyika
katika magazeti mbali mbali ikiwemo na
gazeti la Serikali la Zanzibar leo.
Alisema
kuwa
wameweza kugundua makosa mengi yakiwemo udondoshaji wa viambishi katika
vichwa vya habari , vitenzi kudondosha wakati jambo ambalo
linachangia mkanganyiko kwa msomaji wa gazeti hilo
Alisema kuna
makosa ya kijumla kwa upande wa viambishi hata katika matini vipashio katika uwambishaji
wa maneno,tahajia pamoja na utaratibu wa uundaji wa maneno .
Alielezea kuwa
Kiswahili kimesanifiwa kuwa lugha ya Kiswahili
sanifu na lahaja zipo kwa lengo la kuusaidia
uhai wa lugha hiyo kwa kuengeza misamiati.
Akizungumzia
kwa upande wa Radio jamii alisema Watangazaji hawajakatazwa kutumia lugha zao
kupitia katika vituo vya jamii kwa lengo la mafahamiano ya lugha na jamii husika, sio kwa radio za kitaifa ambazo
zinawasikilizaji wengi.
Nae Katibu Mtendaji
wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Omar Said
Ameir alisema katika kuimarisha na
kujenga upendo na wahariri, watayarishaji vipindi pamoja na watangazaji
wameandaa mashindano ya matumizi ya lugha sahihi ya Kiswahili sanifu kwa vyombo
mbali mbali vya habari, kukusanya vipindi vyao vilivyoanzia Januari mosi hadi Januari
31 mwaka 2020 vitakavyoshinda vitapatiwa
tunzo maalum ya ushindi huo .
Mkutano wa siku
moja wa Wahariri wa Vyombo mbali mbali umetayarishwa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo Dk Juma Mohamed Salum akitoa hotuba ya
Makaribisho katika Mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na
Matumizi ya kiswahili sanifu katika Uandishi wa Habari hafla
iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale
Kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar Mwanahija Ali Juma katikati
akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa katika Mkutano wa
Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na Matumizi ya kiswahili sanifu
katika Uandishi wa Habari hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo
akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa
Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na Matumizi ya kiswahili sanifu
katika Uandishi wa Habari hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...