Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo (Januari 07, 2020) imekutana na wadau wa Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani humo.
Mkutano huo ambao umefunguliwa na kuendeshwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage umehudhuriwa na wadau mbalimbali.
Wadau waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa,Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wawakilishi wa makundi maalum ya Watu wenye Ulemavu, Vijana na Wanawake, Wanahabari na Wazee wa Kimila.
Jaji Kaijage amesema Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam, unatarajiwa kufanyika kwa siku 7 kuanzia Februari 14 hadi 20, 2020, sambamba na mkoa wa Pwani.
Viongozi wengine wa Tume waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Wajumbe wawili wa Tume, Mhe. Jaji (Mst) Thomas Mihayo na Mhe. Asina Omari. Wengine ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile na Mkurugenzi wa Daftari na Tehama, Bw. Martin Mnyenyerwa.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulizinduliwa tarehe 18 Julai 2019 Mkoani Kilimanjaro na mpaka sasa umefanyika kwenye mikoa 23 ya Tanzania Bara, Halmashauri mbili za Mkoa wa Morogoro na mikoa mitano (5) ya Tanzania Zanzibar.
Uboreshaji wa Daftari kwa sasa unaendelea Mkoani Morogoro (kwa halmashauri zilizosalia). Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam utahitimisha zoezi hilo kwa awamu ya kwanza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...