Na Mwandishi Wetu, Michuzi Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri  Charles Kitima amesema mataifa ya nje yamefanikiwa kwenye mapambano dhidi ya unyapapaa kwa watu wenye virusi vya U kwasababu wameihusisha sayansi na dini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioshirikisha viongozi wa dini wa kitaifa, Serikali, wafadhili pamoja wadau wengine wa mapambano dhidi ya Ukimwi,  Padri Kitima amesema kuwa lengo la kukutana kwa wadau hao ni kujadili namna watakavyotekeleza mpango mkakati wa namna ya kupunguza unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Mpango huo unatekelezwa na  Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA), wakishirikia na Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID), ukiwa na lengo kupunguza unyanyapaa ili kufikia malengo ya 95,95,95. Mkutano huo ulijikita pia kuwajengea uwelewa wa mkakati huo viongozi mbalimbali wa dini, wadau na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya ukimwi.

Akichangia katika mkutano huo, Padri Kitime amesema sayansi na dini  vinakwenda pamoja  na kwamba viongozi hao wa kiroho  wanaaminika kwa sababu wanaokena ni walinzi wa uhai unaohusisha na Mungu.
 Padri Kitime amefafanua kwamba  licha ya mataifa hayo kuwa na uwezo mkubwa kisayansi na kiteknolojia, bado  dini ina nafasi kubwa  katika mapambano dhidi ya unyanyapaa. “Ndiyo maana kiongozi wa dini akisema nikikuwekea mkono utapona, watu watakuja na wataacha kwenda kupima sambamba na kuacha kunywa dawa huwezi kuamini. Yote hii kwa sababu sayansi na teknolojia haijaweza kupenya,” amesema

Ameongeza kuwa "Lakini huku kwetu hasa maeneo ya vijijini sayansi na teknolojia haipewi nafasi  na ndio maana wakati mwingine usipo waelimisha viongozi unaweza ukasabaisha Taifa kuongozwa kutokujua.

Amefafanua baadhi yao wamesoma kwenye elimu ya chini na uwezo wao mdogo huku akitolea mfano taifa la Marekani ambalo raia wake ni wagumu kudanganywa huwezi ukawaambia waombewe bila kupima kwanza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Alhaj Nuhu  Mruma aliungana na  Pardi Kitime na viongozi wengine  waliochangia katika mkutano huo akisema afya ya waumini wa dini mbalimbali ni muhimu kama  Serikali unavyojenga uchumi wa nchi.

“Kwenye viongozi wa dini mambo yakikaa vizuri yanakuwa safi, lakini mambo yakikaa vibaya sauti zao zinaweza kusababisha fikra zao watu kwa haraka .Tuna nia nzuri na jambo hili na tunaliungana mkono ili lisonge mbele na kufanikiwa. Katika mkakati kupima ni jambo muhimu sana.
,” amesema Mruma

 Wakati huo huo Msimamizi wa Mradi USAID ,  Gray  Saga amesema changamoto iliyopo ni  namna gani kushirikiana  viongozi   wa dini na mashirika akisema  mwanzoni mchakato huu ulikuwepo lakini  kipindi cha siku za hivi karibuni umekuwa ukisuasua.

Saga amesema kuwa hivi sasa mambo yanakwenda vizuri  baada ya kutiliwa  mkazo na kwamba katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI  shirika hilo limelenga kuwapata wanaume na watoto ili wapime na kuingizwa kwenye dawa  na kufubaza virusi Ili kupunguza maambukizi mapya.

Ameongeza kuwa changamoto iliyopo ni matumizi sahihi ya dawa na  ujumbe unaotolewa na wadau  mbalimbali yakiwemo  mashirika na viongozi wa dini ambao muda mwingine wanaaambiwa  watu waende wataombewa .

“Mtu akiambiwa hivyo anaamini, mnadhani mtaona namna gani tukishirikisha viongozi wa dini tutaweza kupiga hatua. Jambo jingine ni unyanyapaa ambalo NACOPHA wameshilikia bango ni moja ya dhumuni la kikao hichi.

Kwa mujibu wa Saga amesisitiza kwamba Serikali ya Marekani ipo tayari kushirikiana Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na viongozi wa dini katika kuhakikisha juhudi za kupambana na unyanyapaa na maambukizi ya mapya ukimwi yanapiga hatua.

Katika mafunzo hayo Mathew Kawogo (NACOPHA) aliwapitisha wadau hao kwa kuwaelezea hali ya ukimwi pamoja na unyanyapaa nchini Tanzania sambamba na malengo na vipaumbele katika kuhusisha taasisi na viongozi wa dini, ikiwa lengo kuu ni kutokomeza unyanyapaa.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ukimwi, Kifua Kikuu (TB )na dawa za kulevya , Oscar Mukasa  amesema vyombo vya habari  na taasisi za dini ni mhimili ya ziada katika mchakato huo ili kuleta hamasa kwa Watanzania kuhusu mpango huo. Ameshauri pia mpango wa kupambana na TB uendane na ukimwi kwa kuwa vipo pamoja

Mkurugenzi wa Kinga  wa Wizara ya Afya  Dr. Leonard Subi , ameushukuru uongozi wa Nacopha  katika utekelezaji wa mpango  huo unaokwenda sambamba na utoaji wa ushauri  akisema utakuwa chachu kubwa kwenye ngazi ya vijiji, vitongoji na kata.

 Dk.Subi amesema kuwa jambo kubwa  kuwakutanisha pamoja viongozi wakuu wa mihimili yote na kuweka mikakati ya pamoja  katika mapambano dhidi ya unyanyapaa.

 “Ili unyanyapaa uwe ni entry point ya mapambano dhidi ya magonjwa haya makubwa, kama Taifa na utengenezwe ujumbe mahususi wa kitaifa,",amesema na kuongeza takwimu za kitaifa zinasema vijana ndio kundi linaloathirika zaidi, hivyo jamii inapaswa kuliangalia kwanza hili kundi.

Amesisitiza ajenda kuu ya Serikali ni kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 na kwamba tupotoka ni mbali na Ukimwi sio mpya huku akielezea takwimu zinasema tulitoka ulikuwa kwa asilimia 7.1 na sasa tupo kwenye asilimia  4.7."Tunashukuru wanasayansi kwa kutuletea matumaini kwa kuweza kutuletea dawa zinazofanya watu waweze kuishi. Pia aliongezea kuwa mchango wa Serikali katika mapambanoya UKIMWI ni mkubwa sana pamoja na wafadhili."
 Rev. Christosiler Kalata kutoka Mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya UKIMWI (Tanzania Network of Religious Leaders Living with HIV/AIDS) akichangia hoja wakati wa mjadala kwenye Mkutano wa wadau uliowashirikisha viongozi wa juu dini wa kitaifa, serikali, wawakilishi wa bunge, wadau wa UKIMWI mbalimbali kwa ajili ya kujadili namna watakavyotekeleza mpango mkakati wa Nacopha wa kupunguza unyanyapa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
 Oscar Mukasa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ukimwi, TB na dawa za kulevya akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo

 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanyika kwa mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) Padri Charles Kitima akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Wadau wakiendelea na majadiliano wakati wa mkutano uliowakutanisha kujadili namna gani ya kukomesha unyanyapaa kwa watu wanaishi na virusi vya Ukimwi .Wadau hao wamekutana leo jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...