Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) na Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Afrika (UNHCR) zimepongeza hatua ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na shauku huko Sudan Kusini.

Filippo Grandi, Kamishna wa UNHCR amesema katika taarifa kuwa, serikali mpya inahuisha matumaini ya amani na mustakabali mzuri kwa watu wa nchi hiyo ambao wameteseka kutokana na mgogoro wa muda mrefu.

Nayo IGAD imeahidi kuendelea kuiunga mkono serikali ya Juba ili kuhakikisha kuwa taifa hili linakuwa na amani ya kudumu, utulivu na ustawi. Umoja wa Afrika pia umepongeza hatua ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kiataifa nchini Sudan Kusini.

Hatimaye baada ya ngoja ngoja, Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Sudan Kusini iliundwa hapo jana baada ya kinara wa upinzani, Riek Machar kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Salva Kiir.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...